Sudan: Jeshi na RSF zakubaliana kuwalinda raia wakati huu mapigano yakiendelea
NAIROBI – Jeshi na wanamgambo wa RSF nchini Sudan, wametia saini mkataba wa kuheshimu hali ya kibinadamu wakati huu mapigano yakiendelea lakini wameshindwa kukubaliana kuhusu kusitisha vita.
Imechapishwa:
Cheza - 01:01
Pande hizo mbili zimekubaliana kuwalinda raia na kuweka mbele maslahi yao mbele, kwa mujibu wa mkataba huo, uliotiwa saini na wawakilishi wa kiongozi wa kijeshi Abdel Fattah al-Burhan na kiongozi wa kundi la RSF Mohamed Hamdan Daglo.
Makubaliano hayo, yanamaanisha kuwa pande hizo mbili, zitawaruhusu raia kukimbilia katika maeneo salama, watakayochagua.
Hii imekuja baada ya wawakilishi hao kuendelea na mazungumzo yanayoendelea jijini Jeddah, chini ya uangalizi wa Saudi Arabia na Marekani.
Licha ya kutiwa saini kwa mkataba huo, ripoti zinasema, makubaliano hayo hayajaanza kuheshimiwa, wakati huu mapigani yakiendelea jijini Khartoum.
Wajumbe wa Marekani kwenye mazungumzo hayo, wanasema mambo bado ni magumu, lakini hatua ya kukubaliana kuheshili hali ya kibinadamu ni muhimu.
Kwa karibu mwezi mmoja sasa, vita vinavyoendelea vimesababisha vifo vya watu 750 na kuwaacha wengine zaidia ya Elfu tano, wakiwa na majeraha na Laki tisa kukimbia makaazi yao.