Pata taarifa kuu

Sudan: Mapigano yaendelea kuripotiwa, mazungumzo yakiaanza nchini Saudia Arabia

NAIROBI – Nchini Sudan, mapigano zaidi yameripotiwa jijini Khartoum wakati wajumbe kutoka upande wa jeshi na wanamgambo wa RSF wakikutana kwa ajili ya mazungumzo nchini Saudi Arabia.

Mapigano yanaripotiwa kuendelea nchini Sudan wito wa kusitishwa ukiendelea kutolewa
Mapigano yanaripotiwa kuendelea nchini Sudan wito wa kusitishwa ukiendelea kutolewa AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya nje ya Saudi Arabia katika taarifa yake imesema, baada ya kuanza kwa mazungumzo ya awali, Jumamosi iliyopita, mazungumzo hayo yataendelea katika siku zijazo kwa lengo la kumaliza vita ambavyo vimeendelea kwa wiki ya tatu sasa.

Aidha, Mawaziri kutoka nchi za Kiarabu waliokutana jijini Cairo, wamekubaliana kuendelea kufuatilia kwa karibu kinachoendelea nchini Sudan kwa lengo la kupata suluhu ya kusitisha mapigano yanayoendelea ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia.

Nchi za kiarabu zimekuwa zikifanya juhudi kurejesha amani nchini Sudan
Nchi za kiarabu zimekuwa zikifanya juhudi kurejesha amani nchini Sudan REUTERS - AMR ABDALLAH DALSH

Tayari Saudi Arabia, ambayo ni mwenyeji wa mazungumzo kati ya pande hizi mbili, imesema iattoa Dola Milioni 100 kusaidia, kupatikana kwa misaada ya kibinadamu.

Martin Griffiths, Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na misaada ya kibinadamu naye pia yupo nchini Saudi Arabia kusaidia katika mazungumzo ya kusitisha vita ambayo vimesababisha zaidi ya vifo 700 na watu zaidi ya Laki Moja kukimbia nchi hiyo.

Mamia ya raia wa Sudan wameripotiwa kutoroka nchini humo na kuingia katika mataifa jirani ya Chad na Sudan Kusini
Mamia ya raia wa Sudan wameripotiwa kutoroka nchini humo na kuingia katika mataifa jirani ya Chad na Sudan Kusini AP - Peter Louis

Wito umeendelea kutolewa kwa pande zinazipoigana nchini Sudan kusitisha mapigano na kufanya mazungumzo kama njia moja ya kuepusha taifa hilo kutumbukia katika mzozo wa kibinadamu.

Mamia ya raia wa Sudan wameripotiwa kutoroka nchini humo na kuingia katika nchi jirani kama vile Chad na Sudan Kusini wakihofiwa kushambuliwa katika mapigano yanayoendelea.Tayari nchi za kigeni zimewaondoa raia wake nchini Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.