Pata taarifa kuu

Umoja wa mataifa kutuma ujumbe wake nchini Sudan

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, anajiandaa kutuma ujumbe maalumu nchini Sudan, wakati huu hali ya usalama ikiendelea kuzorota kutokana na mapigano yanayoendelea ambayo yameingia wiki ya tatu.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres AP - Achmad Ibrahim
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huu unatumwa wakati ambappo, licha ya makubaliano ya usitishaji mapigano kwa saa 72, kumeripotiwa mapigano zaidi jijini Khartoum na kwenye maeneo mengine ya nchi.

Kwa hali hii titarajie suluhu yoyote siku za karibuni? Haji Kaburu ni mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Tanzania.

“Suluhu inaweza kupatikana tu pale ambapo makundi haya mawili ambayo yanatafautiana kiitikadi wakati tutaweza kuondoa mkono na ushawishi wa mataifa ya nje ndani ya Sudan.” amesema Haji Kaburu.

00:32

Haji Kaburu kuhusu hali nchini Sudan

Shirika la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema Takriban watu elfu 6 wengi wao wanawake na watoto, wameendelea kukimbia mapigano nchini Sudan na kuelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati, ikiwa ni wiki mbili baada ya kuanza kwa mapigano kati ya jeshi la Sudan na wapiganaji wa RSF.

Fafa Olivier Attidzah, ni Afisa wa shirika hilo anayehusiak na huduma za kibinadamu.

“Watu hawa wengi wao ni watoto na wanawake na wanatuambia kuwa wanaume walibaki upande wa Sudan wakati huo wakimbizi hawa hawataki hata kwenda mbali kutoka katika eneo hili la mpaka.” amesema Fafa Olivier Attidzah.

00:46

Fafa Olivier Attidzah kuhusu wakimbizi wa Sudan

Raia 51 wa Africa Kusini waliokuwa wamekwa nchini Sudan kutokana na vita vinavyoendelea nchini humo wamewasili Afrika kusini, waziri wa maswala ya uhusiano wa kimataifa nchini humo Naledi Pandor akisema za raia 61 wameondolewa na serikali kutoka Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.