Pata taarifa kuu

Sudan: Mapigano yanaripotiwa licha ya makubaliano ya kusitisha vita kwa saa 72

NAIROBI – Licha ya Jeshi la serikali ya Sudan na vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) kuafikiana kuongeza muda wa kusitisha mapigano kwa saa muda wa 72, makabilianoi yamendelea kuripotiwa nchini humo wakati huu kila pande zikiendelea kutuhumiana kwa kukiuka sehemu ya makubaliano hayo.

Wapiganaji wa RSF nchini Sudan
Wapiganaji wa RSF nchini Sudan AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya nchini Sudan inasema kuwa watu 528 wameuawa katika mapigano hayo wengine 4,599 wakiwa wamejeruhiwa, umoja wa mataifa nao ukisema kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka.

Mapigano hayo yalioaanza tarehe 15 ya mwezi Aprili yamezidisha mzozo wa kibindamu nchini Sudan ambapo idadi kubwa ya raia wake walikuwa wanategemea misaada hiyo kabla ya kuzuka kwa mapigano.

Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa jijini  Khartoum Sudan
Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa jijini Khartoum Sudan AP - Marwan Ali

Mapigano ya nchini Sudan yanaathiri nchi jirani kiuchumi

Nchi zinazopakana na Sudan zinakabiliwa na changamoto za kiuchumi kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia katika mataifa hayo wakitokea nchini Sudan ambako kunaendelea kushuhudiwa mapigano.

Kwa mafano, bei ya bidhaa imeripotiwa kupanda kwa asilimia 70 katika muda wa wiki chache hali inayozua wasiwasi kuwa huenda raia nchini humo wakakabiliwa na uhaba wa bidhaa muhimu iwapo idadi ya wakimbizi wanaoingia nchini Chad itaendelea kupanda.

Raia wa Sudan na wale wa kigeni wameendelea kutoroka nchini humo wakihofiwa kuathirika na mapigano yanayoendelea
Raia wa Sudan na wale wa kigeni wameendelea kutoroka nchini humo wakihofiwa kuathirika na mapigano yanayoendelea REUTERS - IHSAAN HAFFEJEE

Hali sawa ni hiyo inashuhudiwa nchini Sudan Kusini, taifa ambalo pia limeripotiwa kupokea idadi kubwa ya raia wa Sudan ya juu wanaokimbia mapigano yanayoendelea nchini mwao.

WFP imerejelea shughuli zake nchini Sudan

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limethibitisha kuwa linarejelea shughuli zake nchini Sudan baada ya kusitishwa tarehe 16 ya mwezi Aprili. Mkurugenzi mkuu wa WFP Cindy McCain ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter.

WFP ilitangaza kusitishwa kwa shughuli zake nchini humo baada wafanyakazi wake watatu kuawaua katika mapigano yanayoendelea nchini humo kati ya makundi mawili ya kijeshi.

Karibia watu 528 wameripotiwa kuuwaua katika mapigano hayo wengine zaidi ya 4,599 wakiwa wamejuruhiwa tangu kuaanza kwa mapigano hayo Aprili 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.