Sudan: Usitishaji mapigano wa saa 72 unaingia siku ya mwisho leo Alhamisi
NAIROBI – Nchini Sudan, usitishaji mapigano wa saa 72 ulioafikiwa kufuatia juhudi za Marekani unaingia katika siku yake ya tatu na ya mwisho Alhamisi hii.
Imechapishwa:
Cheza - 01:04
Licha ya hilo makubaliano hayo hayajaheshimiwa kikamilifu licha ya kushuhudiwa kwa utulivu katika baadhi ya maeneo, huku maeneo mengine mapigano kati ya vikosi vya jenerali Al Burhan na Emeti yakiendelea. Wakati huu jeshi likisema liko tayari kuongeza muda wa usitishwaji wa mapigano.
Katika siku ya tatu ya usitishaji mapigano, makabiliano yameendelea kushuhudiwa katika mji mkuu wa Sudan ambapo ndege za kivita za jeshi ziliruka katika vitongoji vya kaskazini, zikishutumiwa kurusha mizinga mikubwa kuelekea katika ngome za wanamgambo.
Mashuhuda wanasema jiji la Kharthum limeshuhudia utulivu kwa muda mfupi kifuatia makubaliano, ambapo hata hivyo makubaliano hayo yalivunjwa mara moja na kuanza kushuhudiwa kwa mara nyingine tena ubabe katika ya pande mbili zinazokinzana.