Pata taarifa kuu

Sudan: Hakuna ishara ya pande hasimu kufanya mazungumzo : UN

NAIROBI – Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Volker Perthes, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, hakuna dalili za Majenerali wawili wanaongoza mapambano nchini Sudan Abdel Fattah al-Burhan na Mohamed Hamdan Dagalo wako tayari kwa ajili ya mazungumzo, ili kumaliza mapigano.

Magenerali wawili wanaopigana nchini Sudan
Magenerali wawili wanaopigana nchini Sudan AFP - ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Pande hizo hasimu zimekubali kusitisha makabiliano katika kipindi cha saa 72, mapigano yakionekana kuendelea katika baadhi ya maeneo nchini humo.

“Majenerali hawa wawili wanaendelea na shutuma za ushindani na kutoa madai pinzani ya udhibiti muhimu bado hakuna kuwa wako tayari kujadiliana kwa kina.” amesema Volker Perthes.

00:26

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Volker Perthes

Perthes ametoa kauli hiyo, wakati huu utulivu ukishuhudiwa baada ya pande hizo mbili kukubaliana kusitisha mapigano kwa saa 72 baada ya ushawishi wa Marekani.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress amesema, mzozo huo huenda ukasambaa iwapo suluhu haipatikani.

“Siku hizi kumi za vurugu na machafuko zinavunja moyo, vita vya muda mrefu, vita vya muda mrefu vya kiwango hiki ni vigumu kuvumilia na kufikiria.” ameeleza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress.

00:32

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress

Mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF wamesabusha vifo vya zaidi ya watu 400, na wengine zaidi ya Elfu tatu wakiyakimbia wakijeruhiwa.

Mataifa mbalimbali ya kigeni, yameendelea kuwaondoa raia wake nchini humo.

Wakati huu pia kukiripotiwa kusitishwa kwa mapigano kati ya pande hizo mbili za kijeshi, wito umeendelea kutolewa kwa kuheshimiwa kwa makubaliano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.