Pata taarifa kuu

Raia wa Sudan Kusini warejea nchini mwao wakitokea Sudan

NAIROBI – Raia wa nchi jirani ya Sudan Kusini, ni miongoni mwa waafrika wanaorudi katika nchi zao, kufuatia mapigano kati ya jeshi la taifa la Sudan na wanamgambo wa RSF, waliokubali kusitisha vita kwa saa 72.

Maelfu ya raia wa kigeni wanaoishi nchini Sudan wameendelea kuondoka wakati huu mapigano yakiripotiwa kusitishwa kwa muda
Maelfu ya raia wa kigeni wanaoishi nchini Sudan wameendelea kuondoka wakati huu mapigano yakiripotiwa kusitishwa kwa muda AFP - ABUBAKARR JALLOH
Matangazo ya kibiashara

Raia wa nchi jirani ya Sudan Kusini, ni miongoni mwa waafrika wanaorudi katika nchi zao, kufuatia mapigano kati ya jeshi la taifa Sudan na wanamgambo wa RSF, waliokubali kusitisha vita kwa saa 72.

Atem Jok,amekuwa akiishi jijini Khartoum, amewasili jijini Juba, ni miongoni mwa maelfu ya wananchi wa Sudan Kusini, waliokimbia vita katika nchi jirani ya Sudan, waliyojitenga nayo mwaka 2011.

“Tuliishi kwa siku kadhaa bila maji na umeme. Maduka yote ya kuuza vyakula yalikuwa yamefungwa. Ilibidi tusubiri hadi wanajeshi wa serikali na wanamgambo wanaongozwa na Hemetti, naibu wa kiongozi wa kijeshi Abdel Fattah Burhan, walipowakubalia walionaswa na mapigano waondoke.” amesema Atem Jok.

00:20

Atem Jok,amekuwa akiishi jijini Khartoum

Baadhi ya raia wa Sudan Kusini, kama Thon Garang, wamekuwa wakitegemea  huduma za Hospitali za jiji la Khartoum kwa ajili ya matibabu. Vita vimesambaratisha huduma muhimu kukwama, hana budi kurudi nyumbani.

“Ilitulazimu sisi waliokuwa wakiondoka kusaidiana na kutimia kile tulichokuwa nancho kuondoka Sudan. Kuna wananchi wengi wa Sudan Kusini, labda maelfu ambao wamekuwa Khartoum kupata matibabu ya magonjwa mbalimbali.” ameelezaThon Garang

00:17

Thon Garang, raia wa Sudan Kusini ambaye amerejea kutoka Sudan

Ripoti zinasema, maelfu ya raia wengine wa Sudan Kusini, wamekwama katika mji wa Paloch na miji mingine, katika jimbo la Upper Nile, bila chakula, maji na makaazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.