Pata taarifa kuu

Kundi wa Wagner lakanusha wapiganaji wake waliuawa nchini Mali

NAIROBI – Mkuu wa kundi la wapiganaji wa kijeshi wa Urusi maarufu Wagner, Yevgeny Prigozhin, Jumatano, Aprili 26, amekanusha madai kuwa wanachama wake ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio la kijihadi katikati mwa Mali.

Mkuu wa "Wagner" Yevgeny Prigozhin huko Moscow, Aprili 2023
Mkuu wa "Wagner" Yevgeny Prigozhin huko Moscow, Aprili 2023 © AP
Matangazo ya kibiashara

Kundi linalounga mkono dini ya Kiislamu na Waislamu, GSIM, limedai kutekeleza shambulio hilo la kujitoa mhanga katika eneo la Sevare Jumamosi, Aprili 22.

GSIM, ilithibitisha vifo vya wapiganaji wake 15 katika shambulio hilo, kadhalika likisema makumi ya wanajeshi wa Mali na wapiganaji kutoka Urusi waliuawa au kujeruhiwa.

Naweza kusema, kwamba taarifa ninayo ni kuwa hakuna mpiganaji hata mmoja wa Wagner ambaye aliuawa huko Sevare, Prigozhin amesema kwenye mtandao wake wa kijamii akijibu swali kutoka shirika la habari la AFP.

Kundi la Wagner limeripotiwa kuwepo katika nchi zenye migogoro kama Ukraine, Syria, Libya, Mali, na Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo limetuhumiwa kutekeleza dhulma.

Jeshi la Mali limekuwa likishirikiana na wapiganaji wa Wagner tangu mwaka 2022.

Katika shambulio hilo la Jumamosi wiki iliyopita, serikali ya Mali ilitangaza kuuawa kwa raia 10 na wanajeshi watatu, pamoja na makumi ya wanajihadi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.