Pata taarifa kuu

Sudan: Hatua ya usitishaji mapigano kwa saa 72 imeanza

NAIROBI – Nchini Sudan, hali ya usitishaji mapigano imeanza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo, baada ya mazungumzo yaliosimamiwa na Marekani, ambapo majenerali wawili wanaohasimiana kwenye mzozo huo wamekubali kusitisha mapigano kwa siku tatu.

Raia wa kigeni wameendelea kuondolewa nchini Sudan wakati huu mapigano yakisitishwa kwa saa 72
Raia wa kigeni wameendelea kuondolewa nchini Sudan wakati huu mapigano yakisitishwa kwa saa 72 AFP - ADJ LAURE-ANNE MAUCORPS EP DERRI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, amesema hatua hiyo imeafikiwa baada ya mazungumzo ya saa 48 kati ya pande hizo mbili, wakati pia akielezea hofu yake juu ya kuhusishwa kwa kundi la wapiganaji wa Urusi Wagner.

“Inasalia muhimu sana kwa mataifa kutumia ushawishi wowote walio nao kujaribu kuelekeza Sudan kwa njia inayofaa.” amesema Antony Blinken waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani.

00:34

Antony Blinken waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani

Katika siku zilizopita, makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano kati ya pande hizo mbili hayakuheshimiwa.

Wakati hayo yakijiri, shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty limetoa wito wa raia wanaotaka kuondoka kupewa njia salama kufanya hivyo, wakati huu hali ya kibinadamu ikiripotiwa kuwa mbaya katika mji wa Khartoum na maeneo ya Darfur.

Abdulahi Hassan ni mtafiti katika shirika la Amnesty International.

“Hali nchini Sudan ni mbaya sana kiasi kwamba watu wamenaswa majumbani na katika majengo mengine na hakuna na hawawezi kuondoka.” ameeleza Abdulahi Hassan, mtafiti katika shirika la Amnesty International.

00:21

Abdulahi Hassan ni mtafiti katika shirika la Amnesty International

Zaidi ya watu 420 wameua na wengine zaidi ya 3,700, kujeruhiwa katika mapigano hayo ya siku kumi.

Hatua hii ya makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano inakuja wakati huu mataifa mbalimbali yakiendelea kuwaondoa raia wake nchini humo.

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu katika taarifa yake limesema kuwa hali ya kibindamu inaendelea kuwa mbaya zaidi nchini Sudan, uhaba wa maji, chakula na dawa ukiripotiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.