Pata taarifa kuu

Sudan: Mapigano yanaendelea, raia wa kigeni wakiondolewa Khartoum

Nchini Sudan, vita kati ya jeshi la kawaida linaloongozwa na Jenerali Bourhane na wanamgambo wa vikosi vya jeshi maalum la RSF vimeingia wiki ya pili. FAS inadai kuwa na udhibiti wa maeneo yote ya kimkakati ya nchi, lakini wanamgambo wa Jenerali Hemetti wanaonekana kuwa wameimarika katika jimbo la Darfur na katika mji mkuu Kharthoum.

Raia wa Kigeni wanaendelea kuondolewa nchini Sudan wakati huu mapigano yakiendelea
Raia wa Kigeni wanaendelea kuondolewa nchini Sudan wakati huu mapigano yakiendelea via REUTERS - SAUDI MINISTRY OF DEFENSE
Matangazo ya kibiashara

Katika mzozo huu, ambapo pande zote mbili zinazidisha taarifa potofu, mapigano tayari yamesababisha zaidi ya watu 413 kuuawa na 3,551 kujeruhiwa, kulingana na Shirika la Afya duniani.

Mapigano yaliendelea hasa huko Darfur, mojawapo ya mikoa maskini zaidi ya Sudan, ambako RSF inaonekana kuwa imara na hali ni mbaya, kulingana na daktari Claire Nicolet wa shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF.

“Kumekuwa na mshikamano, hosipitali zengine zimetupea vifaa na hata madakatari wamekuja kusaidia zaidi, kwa kipindi cha siku sita tumepokea majeruhi zaidi ya mia nne hamsini.” amesema daktari Claire Nicolet kutoka shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF.

00:38

Claire Nicolet kuhusu Sudan

Haya yanajiri wakati huu nchi mbalimbali za kigeni zimeendelea kuwahamisha wanadiplomasia na raia wake, wakati huu mapigano yakiendelea jijini Khartoum kati ya wanajeshi wa serikali na vikosi vya RSF.

Hapo jana Marekani na Uingereza zilitangaza kuwaondoa wanadiplomasia wake nchini humo. James Cleverly ni waziri wa mambo ya nje wa Uingereza.

“Kutokana na kuongezeka kwa ghasia jijini Khartoum na kwa sababu ya vitisho dhidi ya wanadiplomasia, tumechuka uamuzi wa kufunga kwa muda ubalozi wetu jijini Khartoum.” ameeleza James Cleverly ni waziri wa mambo ya nje wa Uingereza.

00:24

James Cleverly ni waziri wa mambo ya nje wa Uingereza kuhusu Sudan

Ufaransa, Ujerumani, Italia na Hispania, ni miongoni mwa nchi ambazo zimewahamisha raia wake nchini humo.

Mapigano yanayendelea nchini Sudan licha ya wito kutoka kwa jamii ya kimataifa ya kutaka kusitishwa jwa makabiliano kati ya pande hizo mbili za kijeshi.

Raia wa kigeni wameendelea kuondolewa nchini Sudan
Raia wa kigeni wameendelea kuondolewa nchini Sudan REUTERS - ALAA AL SUKHNI

Idadi kubwa ya raia wa Sudan wameendelea kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa chakula, maji na dawa katika hosipitali mbalimbali nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.