Pata taarifa kuu

Ethiopia: Waasi wa Oromia wakubali kufanya mazungumzo na serikali

NAIROBI – Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amesema serikali yake imeanza kuzungumza na waasi wa Oromo Liberation Army wanaopatikana katika jimbo la Oromia.

Serikali ya Ethiopia kufanya mazungumzo na waasi wa Oromia
Serikali ya Ethiopia kufanya mazungumzo na waasi wa Oromia AP - Mulugeta Ayene
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili, yanatarajiwa kunza kesho Jumanne nchini Tanzania, ili kumaliza mapigano ya muda mrefu kati ya wanajeshi wa serikali na waasi hao wanaofahamika kwa kifupi OLA.

Kiongozi huyo wa Ethiopia, ameongeza kuwa raia wa nchi yake pamoja na serikali, wanahitaji sana mazungumzo hayo, na ametoa wito kwa pande zote kuhakikisha kuwa mwafaka unapatikana.

Tangu mwaka 2018, waasi hao wamekuwa wakipambana na vikosi vya serikali, baada ya kundi hilo kugawanyika, na kusababisha mauaji katika jimbo kubwa nchini humo  la Oromia.

Waasi hao wamethibitisha kushiriki kwenye mazungumzo hayo, kwa kile wanachosema serikali imekubali masharti hayo na kumshirikisha msuluhishi huru na kusalia wazi,wakati wa mchakato huo wote.

Hata hivyo, kuelekea kuanza kwa mazungumzo hayo, haijafahamika mfumo wa mazungumzo hayo na ni nani atakuwa msuluhishi.

Serikali ya Ethiopia pia imefanya mazungumzo na kundi lengine la TPLF chini ya uongozi wa umoja wa Afrika na kumaliza mzozo wa zaidi ya miaka miwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.