Mapigano nchini Sudan yanaingia wiki ya pili hali ikiendelea kuwa mbaya
NAIROBI – Nchini Sudan licha ya wito wa Kimataifa wa kusitishwa kwa mapigano wakati wa sikukuu ya Eid Fitr, jeshi la taifa na wanamgambo wa RSF wameendelea kupigana, jijini Khartoum na maeneo mengine ya nchi, na kusababisha idadi ya watu waliopoteza maisha kuongezeka.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Cheza - 01:01
Wakaazi wa Khartoum wamelazimika kusalia katika makaazi yao huku wengine wakiendelea kutorokea maeneo salama, huku jeshi na kundi la RSF likipambana kwa risasi na mabomu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Anthiny Blinken walikuwa wametoa wito kwa pande zote kusitisha vita angalau kwa siku tatu katika kipindi hiki cha EID lakini wito wao umepuuzwa.
Huku makabiliano yakiendelea, Shirika ma afya duniani limetoa takwimu mpya, zinazoonesha kuwa, idadi ya watu waliopteza masiha katika mapigan hayo, imeongezeka na kufikia zaidi ya 400 huku wengine zaidi ya Elfu tatu wakijeruhiwa.
Miongoni mwa waliopoteza maisha ni mfanyakazi wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na wahamiaji IOM, ambaye imeelezwa aliuawa baada ya kushambuliwa wakati akielekea katika mji wa Kusini wa El Obeid.
Jeshi linasema kuwa limetuma silaha zaidi na wanajeshi katika barabara za mji wa Khartoum kuwatafuta wanachama wa Kikosi pinzani cha Wanajeshi wa Rapid Support Forces RSF.
Mapingano hayo yameshuhudia vituo vingi vya matibabu vikiathiriwa na kukosa vifaa vya kutosha vya kutibu. Pamoja na Khartoum, eneo la magharibi la Darfur, pia limeathiriwa vibaya na mapigano.