Pata taarifa kuu

Makabiliano makali yanaripotiwa nchini Sudan licha ya wito wa kusitishwa

NAIROBI – Nchini Sudan, makabilianao yamendelea kushudiwa kati ya pande mbili hasimu za kijeshi, milio ya risasi na milipuko mizito ikisikiza katika mji mkuu wa Khartoum, wakati huu wito  kutoka kwa jamii ya kimataifa wa kutaka kusitishwa kwa mapigano hayo ukionekana kutoheshimiwa.

Raia wa Sudan wanakabiliwa na ugumu wa kupata bidhaa muhimu kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya vikosi viwili vya jeshi.
Raia wa Sudan wanakabiliwa na ugumu wa kupata bidhaa muhimu kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya vikosi viwili vya jeshi. AP - Marwan Ali
Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres alikuwa amezitaka pande hizo zinazozozana kusitisha makabiliano haswa wakati huu jamii ya waisilamu nchini humo wakimaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Hatua ya kusitishwa kwa mapigano pia ingetoa nafasi ya kuwezesha misaada ya kibindamu kuwafikia watu waliothirika na mapigano hayo yanayoendelea kati ya vikosi viwili ya jeshi.

Mapigano hayo yanaonekana kushika kasi wakati huu zaidi ya watu 300 wakiripotiwa kuawaua katika machafuko hayo, maelfu ya wengine wakiwa wametorokea katika mataifa jirani wakihofiwa kushambuliwa.

Wakuu wa kijeshi nchini Sudan ambao vikosi vyao vinaendelea kukabiliana
Wakuu wa kijeshi nchini Sudan ambao vikosi vyao vinaendelea kukabiliana AFP - ASHRAF SHAZLY

Kwa mujibu wa madaktari nchini humo, makabiliano mazito yamesikika usiku wa kuamkia siku ya sherehe za Eid al-Fitr, hali inayotishia kulitumbukiza taifa hilo katika mzozo wa kisiasa.

Katibu mkuu wa UN Antonio Guterres na waziri wa mambo ya nje wa Marekani  Antony Blinken  katika nyakati tofauti wametoa wito wa kusitishwa kwa makabiliano kwa anagalau muda wa siku tatu kutoa  nafasi ya kufanyika kwa seherehe za Eid, wito unaonekana kutoheshimiwa.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeonya kuwa mapigano hayo yanaweza kusababisha mamilioni ya raia wa Sudan kukabiliwa na baa la njaa.

Raia wa Sudan wameendelea kukimbia mapigano yanayoendelea
Raia wa Sudan wameendelea kukimbia mapigano yanayoendelea REUTERS - EL TAYEB SIDDIG
Shirika hilo la umoja wa mataifa limesitisha shughuli zake nchini humo baada ya wafanyakazi wake watatu kuawaua siku ya Jumamosi iliyopita.

 

Mkuu wa jeshi la Sudan generali Burhan na kiongozi wa RSF Daglo wametajwa kuzozania mpango ya kutaka vikosi vya RSF kujumuishwa katika jeshi la kitaifa, kipenge muhimu katika kurejesha utawala wa kiraia nchini humo.

 

Mataifa kadhaa tayari yameanzisha mipango ya kuwaondoa raia wake wanaoishi nchini Sudan wengi wakiwa ni wanafunzi kwa hofu kuwa huenda wakaathirika na machafuko yanayoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.