Pata taarifa kuu

Raia wa Sudan wanakabiliwa na uhaba wa mahitaji muhimu mapigano yakiendelea

NAIROBI – Wakaazi wa jiji la Khartoum tangu kuanza kwa vita, sasa wanakabiliwa na ukosefu wa mahitaji muhimu ya kibinadamu kama chakula, maji lakini pia wameshindwa kupata huduma ya afya.

Mapigano yanapoendelea nchini Sudan, raia wanakabiliwa na uhaba wa bidhaa muhimu ikiwemo maji
Mapigano yanapoendelea nchini Sudan, raia wanakabiliwa na uhaba wa bidhaa muhimu ikiwemo maji © Twitter @ayman_amin_/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Vita hivyo, vimesababisha maelfu ya watu kuanza kukimbia jijini Khartoum. Wanaoamua kubaki wanasema kwa siku kadhaa sasa   hawana umeme. Lual Akwol, ni raia wa Sudan Kusini, ambaye ni Mwalimu jijini Khartoum.

“Hakuna maji watu wanatembea kila mahali wakitafuta maji. Hakuna umeme. Umeme umekatwa. Miliyo ya risasi inaendelea inasikika Kila mahali.” Amesema Lual Akwol.

00:12

Lual Akwol, raia wa Sudan Kusini

Farid Aiywar ni mfanyakazi wa shirika la msalaba mwekundi jijini Khartoum, anasema wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wameendelea kupata changamoto ili kuwasadia watu.

“Ukweli ni kwamba kwa sasa imekuwa vigumu kusambaza misaada kwa watu wanaohitaji mjini Khartoum na vitongoji vyake.” ameeleza Farid Aiywar.

00:26

Farid Aiywar, mfanyakazi wa shirika la msalaba mwekundi jijini

Mashirika ya Kimataifa kama OCHA na WHO yanaonya kuwa iwapo suluhu ya haraka haipatikana kuhusu mzozo huu, itakuwa vigumu kuwasaidia wakaazi hasa wa Khartoum katika nchi hiyo ambayo watu Milioni 11 wanahagaika kupata chakula kima siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.