Pata taarifa kuu

Sudan: Jeshi limeendelea kupigana na vikosi vya RSF kwa siku ya tano sasa

NAIROBI – Nchini Sudan  kwa siku ya tano leo, jeshi limeendelea kupambana na vikosi maalum vya RSF jijini Khartoum, baada pande zote kushindwa kutekeleza maelewano wa kusitisha vita kwa saa 24 hapo jana, wakati huu idadi ya watu waliopoteza maisha ikiongezeka na kufikia zaidi ya 200.

Raia wa Sudan akikadiria hasara kutokana na mapigano kati ya jeshi na RSF
Raia wa Sudan akikadiria hasara kutokana na mapigano kati ya jeshi na RSF © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mapigano makali yameendelea huku ripoti zikisema, makundi hayo mawili yanakabiliana katika makaazi ya watu wengi jijini Khartoum.

Shirika la afya duniani, linasema watu zaidi ya watu 270 mpaka sasa wamepoteza maisha na inahofiwa kuwa idadi hiyo itaongezeka iwapo vita havitakomeshwa.

Saa chache zilizopita, wanamgambo wa RSF walisema wako tayari kusitisha vita kwa saa 24 zijazo kunazia saa 12 jioni saa za Khartoum, lakini jeshi halijasema chochote.

Wakati Jumuiya ya Kimataifa ikiendelea kushinikiza, pande mbili zinazopigana kuweka silaha chini, maelfu ya watu jijini Khartoum wanakimbilia maeneo salama kwa hofu ya kushambuliwa.

Mabalozi wa nchi mbalimbali  kutoka nchi za Magharibi nchini humo, wametoa taarifa ya pamoja wakitaka jeshi la RSF kukubali kusitisha vita na kuheshimu sheria za Kimataifa.

Rais wa Kenya William Ruto ametoa taarifa, akizitaka pande mbili zinazopigana kuheshimu wito wa Jumuiya ya nchi za IGAD, wa kusitisha vita, kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia walengwa na kushirikiana na viongozi wa Jumuiya hao watakapozuru Khartoum.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.