Pata taarifa kuu

IGAD yatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano Sudan

NAIROBI – Mapigano makali yameendelea kuripotiwa jijini Khartoum,nchini Sudan, licha ya kusitishwa kwa muda siku ya jumapili ili kutoa fursa ya kuwasaidia waliojeruhiwa katika mapigano hayo yaliozuka siku ya Jumamosi.

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na kiongozi wa vikosi maalum nchini humo RSF Generali Mohamed Hamdan Daglo (Hemedti), jijini Khartoum Juni 8, 2022.
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na kiongozi wa vikosi maalum nchini humo RSF Generali Mohamed Hamdan Daglo (Hemedti), jijini Khartoum Juni 8, 2022. AFP - ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya waliofariki imefikia 97 kwa mujibu wa muungano wa madaktari nchini humo.

Mapiganao yanaripotiwa kuendelea kwa siku ya tatu, na kwa mujibu wa madaktari, mamia ya watu wamejeruhiwa, wakati huu shirika la afya duniani WHO, likionya kuwa baadhi ya hospitali katika mji wa Khartoum zinazopokea majeruhi hazina damu ya kutosha na vifaa vinavyohitajika.

Mapigano haya yamesababisha shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, kutangaza kusitisha shughuli zake katika taifa hilo, haswa baada ya wafanayakazi wake watatu kuuawa.

Mapigano kati ya jeshi la sudan na Vikosi vya (RSF) yamezua hisia na wasiwasi wa kikanda, ikiwa ni pamoja na kufungw akwa mipaka nan chi jirani za  Misri na Chad.

Vikosi vya RSF vinavyoongozwa na Mohamed Hamdan Daglo vimesema kuwa vimedhibiti makao makuu ya rais, uwanja wa ndege wa Khartoum na maeneo mengine ya kimkakati, lakini hata hivyo jeshi limesisitiza kuwa bado lina udhibiti.

Nchi mbali mbali zikiwemo Uingereza, China, Umoja wa Ulaya na urusi zimeendelea kutoa wito wa kusitishwa mapigano

Kwa upande mwengine Jumuiya ya maendelea Afrika Mashariki na pemebe ya Afrika IGAD hapo jana imetoa wito wa kusitishwa mapigano nauhasama kati ya pande mbili zinazohasimiana nchini Sudan.

Katika mkutano uliofanyika kwa njia ya video, viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo walikubaliana kuwatuma marais wa Kenya, William Rutoi, wa sidan Salva Kiir na Ismaïl Omar Guelleh wa Djibout ili kusiadia katika kutafuta suluhu.

William Ruto ni rais wa Kenya.

“Kama IGAD na kama mkuu wa nchi tunaomba kusitishwa kwa uhasama unaoendelea Sudan.”amesema rais William Ruto.

00:39

Rais William Ruto kuhusu Sudan

Mweneykiti wa umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, pia anatarajiwa kusafiri nchini Sudan kukutana na pande zinazohasimiana katika mzozo huo ili kuzishawishi kusitisha mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.