Pata taarifa kuu
MAPIGANO-USALAMA

Sudan: WFP yasitisha msaada wake baada ya vifo vya wafanyakazi watatu

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limetangaza Jumapili kusitishwa kwa shughuli zake nchini Sudani baada ya vifo vya wafanyakazi watatu waliokuwa wanafanya kazi kwa shirika hili maalum la Umoja wa Mataifa ambalo makao makuu yake yapo Roma

Khartoum, Sudan, Aprili 16, 2023: Kwa kukata kuhatarisha maisha yao kutokana na kuwepo kwa wanajeshi kwenye paa za nyumba, wakati mwingine raia hulazimika kusalia makwao. Sudan imekuwa katika mzozo wa wazi tangu Jumamosi kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa SFR.
Khartoum, Sudan, Aprili 16, 2023: Kwa kukata kuhatarisha maisha yao kutokana na kuwepo kwa wanajeshi kwenye paa za nyumba, wakati mwingine raia hulazimika kusalia makwao. Sudan imekuwa katika mzozo wa wazi tangu Jumamosi kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa SFR. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

"Tunalazimika kusitisha shughuli zetu kwa muda nchini Sudani wakati wa kutathmini hali ya usalama," amesema Mkurugenzi wa PAM Cindy McCain, akinukuliwa katika taarifa. Wafanyakazi watatu wa WFP wameuawa katika mapigano ambayo yamekuwa yakiongezeka nchini Sudan tangu Jumamosi kati ya vikosi vya msaada wa haraka (FSR) vya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, anayejulikana kama "Hemedti", na Jeshi la serikali,  mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika katika nchi hii ya Afrika Kaskazini-Mashariki ametangaza siku ya Jumapili.

Waliuawa "Jumamosi wakitekeleza kazi yao huko Darfur-Kaskazini", huko Magharibi karibu na Chad, ambayo ilifunga mpaka wake Jumamosi kwa sababu ya vurugu, Volker Perthes anabainisha katika taarifa. Anaongeza kuwa "majengo ya kibinadamu yamelengwa na mapigano na mengine yameporwa huko Darfur", ngome ya kihistoria ya kikosi cha FSR. WFP inabainisha kuwa moja ya ndege zilizotumiwa kwa shughuli zake pia iliharibiwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum.

"WFP inajishughulisha na msaada kwa raia wa Sudan ambayo inakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula, lakini hatuwezi kufanya kazi yetu, ambayo huokoa maisha, ikiwa usalama wa timu zetu na washirika haujazingatiwa", amesema Bi McCain. "kupoteza maisha yetu katika shughuli za kibinadamu hakukubaliki na ninaomba hatua za haraka kuhakikisha usalama wa wale ambao bado wapo," ameongeza.

"Wafanyakazi wa mahirika ya kibinadamu hawana upande wowote wanaoegemea, kwa hivyo hawapaswi kulengwa. Kuhatarisha timu zetu hufanya kuwa haiwezekani kufanya kazi salama, "amesema McCain, akiwaomba wahusika katika mgogoro kupata makubaliano ya" kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wa mashirika ya kibinadamu kwenye uwanja wa mapigano ". Hii itawezesha"kuendelea na msaada wa kibinadamu ambao huokoa watu nchini Sudani. Inaendelea kuwa kipaumbele chetu kikuu, "amehitimisha mkurugenzi wa WFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.