Pata taarifa kuu

Sudan: Mapigano yaripotiwa kati ya kikosi maalum na jeshi la serikali

NAIROBI – Milio ya risasi na milipuko imesikika katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, baada ya siku kadhaa za mvutano kati ya kikosi kikosi maalum cha jeshi la RSF na jeshi la nchi hiyo.

Mapigano yaripotiwa kati ya kikosi maalum na jeshi la serikali nchini Sudan
Mapigano yaripotiwa kati ya kikosi maalum na jeshi la serikali nchini Sudan AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Mzozo huo unahusu mpito unaopendekezwa kwa ajili ya kurejeshwa kwa utawala wa kiraia. Milio zaidi ya risasi imesikika karibu na makao makuu ya jeshi katikati mwa jiji la Khartoum.

Kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) kinasema kimechukua udhibiti wa uwanja wa ndege na ikulu ya rais hali inayotishia kuzua mzozo zaidi.

Jeshi la Sudan limethibitisha kushambulia kambi za RSF likisema kuwa wapiganaji wa RSF wamekuwa wakijaribu kuyateka makao makuu ya jeshi.

Majenerali wamekuwa wakiendesha nchi, kupitia kile kinachoitwa Baraza Kuu, tangu mapinduzi ya Oktoba 2021.

Kikosi cha RSF kiko chini ya amri ya makamu wa rais wa baraza hilo Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, jeshi nalo likiongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye ni mkuu wa Baraza Kuu.

Hatua iliyopendekezwa ya kufikia serikali ya kiraia iliyopo kwenye mpangilio ni kuunganisha kikosi cha RSF katika jeshi la kitaifa.

RSF kwa upande wake imekuwa ikitaka hatua hiyo kuchelewesha kwa miaka 10, jeshi nalo likisema inapaswa kutokea katika miaka miwili.

Siku ya Alhamisi, RSF ilituma vikosi karibu na kambi ya kijeshi huko Merowe huku hali ya wasiwasi ikiongezeka wiki hii.

Jenerali Burhan alisema yuko tayari kuzungumza na mkuu wake wa pili kutatua mzozo wa nani ataongoza jeshi la umoja katika serikali inayopendekezwa ya kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.