Pata taarifa kuu

Sudan: Watu 24 wauawa katika mapigano ya kikabila Darfur

NAIROBI – Nchini Sudan, mapigano mapya kati ya makundi mawili ya waarabu na waiso waarabu, katika eneo la Darfur yamesababisha vifo vya watu 24, nyimba kadhaa kuchomwa moto na maelfu ya watu kukimbia makazi yao.

Ramani ya eneo la Sudan, Darfur.
Ramani ya eneo la Sudan, Darfur. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Ghasia hizi za hivi punde katika eneo la karibu na mpaka na Chad, zinaripotiwa kuzuka kati ya makundi ya kabila la waarabu na Masalit katika mji wa Foro Baranga, karibu kilomoita 185 kutoka mji Geneina, ambao ni mji mkuu wa Jimbo la Darfur Magharibi. 

Kulingana na Mohammed Hussein Teema, kutoka baraza la Foro baranga, mapigano hayo yalizuka jumamosi iliopita. 

Machafuko haya mpaya yameifanya mamlaka wa Sudan kutangaza kafyu nyakati za usiku pamoja na haliya dharura kwa kipindi cha mwezi mmoja katika jimbo hilo, na kwa sasa hali ya utulivu inashuhudiwa baada ya maafisa wa usalama kutumwa eneo hilo. 

Kwa mujibu wa ofisi ya umoja wa mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu, takriban nyumba 50 katika eneo la Foro Baranga pia zinaripotiwa kuchomwa moto na kusababisha familia elfu nne kusalia bila makaazi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.