Pata taarifa kuu

Wafanyikazi wawili wa missada ya kibinadamu wauawa jimboni Amhara

NAIROBI – Nchini Ethiopia, wafanyakazi wawili wa kutoa misaada kutoka Shirika la Kanisa Katoliki, CRS, wameuawa katika jimbo la Amhara, wakati huu maandamano yakishuhudiwa baada ya serikali kutangaza kuyavunja makundi ya kijeshi kwenye majimbo ya nchi hiyo.

Walinda usalama wakipiga doria katika eneo la Amhara nchini Ethiopia
Walinda usalama wakipiga doria katika eneo la Amhara nchini Ethiopia © REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo katika taarifa yake limesema, Meneja wake wa usalama Chuol Tongyik na dereva Amare Kindeya, walipigiwa risasi na kuuawa Jumapili iliyopita, wakati wakiwa njiani wakielekea jijini Addis Ababa, wakitokea Amhara.

Mauaji hayo yamejiri, baada ya kuzuka kwa maandamano yenye ghasia katika miji mbalimbali ya jimbo la Amhara kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya tangazo kuwa kikosi maalum cha kijeshi cha Amhara kitavunjwa.

Serikali jijini Addis Ababa chini ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed, inasema mabadiliko hayo yanalenga kujenga taasisi moja yenye nguvu kulinda usalama wa nchi hiyo  na kuonya kuwa kuwepo kwa vikosi mbalimbali katika kila jimbo, kunahatarisha usalama wa nchi.

Kufuatia kuzuka kwa vurugu katika jimbo la Amharic, serikali kuu imetangaza marufuku ya matumizi ya pikipiki usiku katika miji ya jimbo hilo, kufungwa kwa maeneo ya burudani ifikapo saa tatu usiku, na watu wamezuiwa kubeba visu na rugu.

Migomo imepigwa marufuku katika jimbo la Amharic na mikutano yypte ya ahadhara ni lazima ipate kibali kutoka kwa viongozi wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.