Pata taarifa kuu

Ethiopia: Abiy Ahamed aapa kupambana na makundi ya kikanda yenye silaha

NAIROBI – Waziri mkuu wa Ethiopia, ameapa kumaliza vikosi vya wanajeshi vya kikanda ambavyo yameundwa na majimbo kadhaa nchini humo, akionya kuwa sheria itachukuliwa kwa yeyote atakayepinga operesheni hiyo.

 Abiy Ahmed, Waziri mkuu wa Ethiopia
Abiy Ahmed, Waziri mkuu wa Ethiopia AP - Mulugeta Ayene
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake iliochapishwa kwenye mtandao wa Twitter waziri mkuu Abiy Ahmed, amesema taifa lake limetipia hali ngumu kutoka baadhi ya vikosi vya kikanda kuhusika katika wizi wa mifugo, ulaguzi pamoja na vizuizi vya barabarani ambavyo ni kinyume cha sheria akisema serikali yake  iko tayari kulipa gharama ya kumaliza hali hiyo hadi pale Ethiopia itakaposhuhudia usalama.

Aidha Kauli ya Abiy inalenga kuhakikisha kwamba vikosi vyote vya kikanda vinajumuishwa kwa jeshi la kitaifa, ili kuzia madai ambayo yamekuwa yakiibuliwa dhidi ya vikosi hivyo kwa ukiuwakaji wa haki za binadamu hasa kile cha jimbo la Amhara.

Katiba ya  Ethiopia inaruhusu majimbo yake 11, kuunda vikosi vya polisi ila si wanajeshi kama ambayo baadhi ya majimbo yamefanya kwa zaidi ya kipindi cha miaka 15 iliopita, hatua ambayo imechangia uhasama baina ya majimbo.

Tangu kuzuka vita jimbo Tigray mwaka 2020, Vikosi vya jimbo la Amhara na wapiganaji wanaojiita Fano, wamekalia eneo la magharibi mwaka Tigray, eneo ambalo limekuwa likizozaniwa na Tigray na Amhara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.