Pata taarifa kuu

Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris kuzuru Tanzania

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ambaye aliwasili Ghana Jumapili anatarajia kuzuru Tanzania siku ya Jumatano wiki hii. Tanzania ndiyo kituo kinachofuata cha makamu wa rais kabla ya kuelekea Zambia.

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akitoa hotuba alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kotoka mjini Accra Machi 26, 2023. Kamala Harris aliwasili nchini Ghana siku ya Jumapili na kesho Jumatano atazuru Tanzania kisha Zambia.
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akitoa hotuba alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kotoka mjini Accra Machi 26, 2023. Kamala Harris aliwasili nchini Ghana siku ya Jumapili na kesho Jumatano atazuru Tanzania kisha Zambia. REUTERS - FRANCIS KOKOROKO
Matangazo ya kibiashara

Kwanza alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani aliyefanya ziara Afrika, lakini sasa ni makamu wa rais na baadaye mwakani rais mwenyewe wa Marekani, Joe Biden anatarajiwa kuja Afrika.

Mfulululizo wa ziara hizi kwa viongozi wakubwa katika utawala wa Marekani unaonyesha mwamko unaokua kwamba Marekani inahitaji kuimarisha ushirikiano wake na bara hilo.

Haya yote yanakuja katika namna ya ushindani unaokua kutoka kwa mataifa mengine yenye nguvu duniani, hasa China na Urusi.

Ziara ya Bii Harris, kulingana na taarifa rasmi, itagusia kuhusu mkutano ujao wa kilele wa mwezi Desemba wa Marekani na Afrika huko Washington ambapo Rais Joe Biden alisema Marekani "imejikita katika mustakabali wa Afrika"

0rodha ya nyimbo anaZosikiliza wakati wa safari yake

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ametoa orodha ya nyimbo 25 za wanamuziki wa Kiafrika ambazo anasikiliza wakati wa safari yake ya sasa barani.

Orodha hiyo ya muziki, yenye jina la "Safari yangu": Ghana, Tanzania, na Zambia," inapatikana kwenye Spotify na ina wanamuziki wengi wa Tanzania.

Baadhi ya wasanii wa Tanzania waliotajwa ni pamoja na Zuchu, Alikiba, Jay Melody, Mbosso, Jux, Darassa, Marioo na Platform.

Muziki ulioimwa kwa ushirikiano kati ya Bien Aime Baraza wa Sauti Sol wa Kenya na msanii wa Tanzania Darassa pia upo kwenye orodha hiyo.

Bii Harris alikutana na baadhi ya wasanii wa Ghana siku ya Jumatatu na kueleza nia yake ya kuwatangaza wasanii wa Kiafrika katika masoko ya kimataifa ili kuwasaidia waweze kufikia wasikilizaji wengi zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.