Pata taarifa kuu

Kenya: unyanyasaji wa kijinsia waripotiwa wakati wa maandamano

NAIROBI – Jumatatu usiku na mtaani kibera wakaazi walikuwa na hofu…..Pindi tu makundi mawili hasimu yalipozozana na kusababishwa kuchomwa moto kwa kanisa la PCEA Kibera Parish na vile vile kuharibiwa kwa msikiti na mali nyingine, wakaazi wakaingiwa na wasiwasi.

Wanawake katika mitaa ya Nairobi wanakabiliwa na changamoto za ukatili wa kimapenzi wakati huu maandamano yakiendelea
Wanawake katika mitaa ya Nairobi wanakabiliwa na changamoto za ukatili wa kimapenzi wakati huu maandamano yakiendelea © Ben Curtis / AP
Matangazo ya kibiashara

Kina mama na wasichana wakidhulumiwa kimapenzi katika hali hii. Hapa baadhi wanasimulia hali ilivyo katika mtaa huu wa Kibera nje kidogo na jiji la Nairobi.

Vita iliendelea mpaka usiku saa mbili hali ilikuwa mbaya sana hapa wakati huo.”wameeleza akina mama wa eneo hili la Kibra.

Japo wengi ambao tulizungumza nao waliogopa kutaja dhulma za kimapenzi na wengine kukana madai hayo, shirika la kutetea haki za kibinadam la Muhuri limethibitisha vitendo hivyo.

Franics Auma ni afisa kutoka shirika la kutetea haki za binadamu la Muhuri.

“Watoto wa kike wameumizwa kupitia unyanyasaji wa kimapenzi kuna visa zaidi ya ishirini sio Kibera peke yake hata maeneo mengine ikiwemo kariobangi.”amesema Franics Auma.

Na huku maandamano mengine yakitarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi, kuna hofu ya ongezeko la dhuluma za kimapenzi kwani wakaazi wa mtaa huu wa kibera wanaishi kwa wasiwasi mkubwa.

“Hatua inafaa kuchukuliwa dhidi ya ukatili wa kimapenzi haswa wakati huu maandamano yanapoendelea.”ameongeza Franics Auma.

Ikiwa maandamano yatazidi kuendela nchini Kenya, basi visa zaidi vya unyanyasi wa kijinsia vitazidi kushuhudiwa kwani ndio mwanzo tu mkoko unaalika maua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.