Pata taarifa kuu

Tshisekedi afanya mabadiliko baraza la mawaziri, Bemba Ulinzi, Kamerhe Uchumi

Mabadiliko madogo ya serikali yametangazwa usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mabadiliko hayo yametangazwa ikiwa imesalia miezi tisa kabla ya uchaguzi wa urais.

Jean-Pierre Bemba ateuliwa kuwa Wazri wa Ulinzi katika serikali mpya ya Sama Lukonde.
Jean-Pierre Bemba ateuliwa kuwa Wazri wa Ulinzi katika serikali mpya ya Sama Lukonde. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Kati ya mawaziri wapya walioteuliwa ni pamoja na makamu wa rais wa zamani (2003-2006) Jean-Pierre Bemba, ambaye ameteuliwa kwenye wizara ya Ulinzi. Kiongozi huyo wa zamani wa kivita, Jean-Pierre Bemba alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 18 jela na Mahakama ya Kimataifa (ICC) kwa uhalifu uliofanywa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kabla ya kufutiwa mashitaka mnamo mwaka 2018, baada ya kuzuiliwa kwa miaka kumi huko Hague.

Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi, wakati DRC, inayopambana na vurugu za watu wenye silaha kwa karibu miaka 30 katika sehemu yake ya mashariki, imeshuhudia ongezeko la mvutano na jirani yake Rwanda, inayoshtakiwa kuunga mkono waasi wa M23 ambao wanakalia sehemu kubwa za mkoa wa Kivu Kaskazini tangu mwaka jana.

Mtu mwengine ambaye ameteuliwa kushikilia wizaya nyeti katika serikali hii mpya ni Vital Kamerhe, mkurugenzi wa zamani wa katika ofisi ya Rais Félix Tshisekedi, aliyehukumiwa mnamo miaka ya 2020 kifungo cha miaka 20 kwa ubadhirifu wa mali ya umma kabla ya kuachiliwa katika ngazi ya rufaa mnamo 2022. Ameteuliwa kuwa waziri wa Uchumi, pia naibu Waziri Mkuu. Kuna manaibu Waziri Mkuu watano.

Mabadiliko haya yalitangazwa kufanyika tangu miezi mitatu, baada ya kujiuzulu mwishoni mwa mwezi Desemba kwaa mawaziri watatu wa mfanyabiashara Moïse Katumbi, mgombea wa uchaguzi ujao wa urais, ambaye alondoka serikalini kwa mshikamano na chama chao cha kisiasa baada ya muungano na serikali kuvunjika.

Uchaguzi ujao wa urais umepangwa kufanyika Desemba 20. Félix Tshisekedi, aliyeko madarakani tangu mwezi Januari 2019, alitangaza kwa miezi kadhaa kwamba atakuwa atawania tea katika uchaguzi huo.

Jean-Michel Sama Lukonde ni Waziri Mkuu tangu mwezi Februari 2021. Rais Tshisekedi alimteua baada ya kuvunjika kwa muungano wao na mtangulizi wake Joseph Kabila.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.