Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-SIASA

Zaidi ya watu 550 wakamatwa nchini Afrika Kusini wakati wa maandamano

Zaidi ya watu 550 walikamatwa nchini Afrika Kusini siku ya Jumatatu, mamlaka imesema, wakati wa maandamano yaliyoitishwa na chama chenye siasa kali za mrengo wa kushoto ambayo yalizua hofu ya kurudiwa kwa ghasia mbaya za mwaka 2021.

Wafuasi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) waliandamana hadi kwenye Nyumba ya Wageni ya rais mjini Pretoria mnamo Machi 20, 2023 wakati wa maandamano yaliyoitishwa na chama chao.
Wafuasi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) waliandamana hadi kwenye Nyumba ya Wageni ya rais mjini Pretoria mnamo Machi 20, 2023 wakati wa maandamano yaliyoitishwa na chama chao. AFP - EMMANUEL CROSET
Matangazo ya kibiashara

Kikosi maalum cha usalama kinachoitwa Natjoints kiliwakamata "zaidi ya waandamanaji 550, miongoni mwa mambo mengine, kwa vurugu kwenye barabara za umma, vitisho, uharibifu, wizi na majaribio ya uporaji", mamlaka imesema katika taarifa yake leo Jumanne. Kikosi cha Natjoints kinajumuisha polisi, jeshi na idara ya ujasusi.

Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), kinachoongozwa na Julius Malema, kiliwataka Waafrika Kusini "kufanya mabadiliko" na kuzuia shughuli zote sncjhini humo iku ya Jumatatu kumtaka Rais Cyril Ramaphosa ajiuzulu. Anachukulia kuwa kuwajibika kwa ukosefu wa ajira uliokithiri (32.9%) unaoathiri uchumi, ukosefu wa usawa unaoendelea kukua na mzozo mkubwa wa umeme ambao unaathiri maisha ya kila siku ya Waafrika Kusini milioni 60 kwa kukatwa mara kwa mara.

Ni waandamanaji elfu chache tu ambao hatimaye waliitikia wito huo, hasa katika mji mkuu wa Pretoria ambako karibu watu 5,000 walikusanyika, waandishi wa habari wa AFP wamebainisha.

Lakini wito huo ulirejesha kumbukumbu za wimbi la ghasia na uporaji ambao uliua zaidi ya watu 350 mwezi Julai 2021. Ghasia hizo, mbaya zaidi tangu kumalizika kwa utawala wa kibaguzi, awali zilichochewa na kufungwa kwa Rais wa zamani Jacob Zuma lakini pia zilikuwa ishara ya hali ya kijamii na kiuchumi ambayo bado iko chini kabisa.

Rais Ramaphosa aliahidi wiki jana kuzuia "machafuko". Polisi walikuwa katika "uhamasishaji wa hali ya juu" kote nchini, wakiungwa mkono na karibu wanajeshi 3,500. Kampuni nyingi za usalama za kibinafsi katika nchi hiyo yenye uhalifu mkubwa zimesaidia na kufanya kama "kuzidisha nguvu katika maeneo mbalimbali".

"Hatua zilizowekwa zimeruhusu biashara na huduma kufanya kazi kwa kiwango cha chini cha matukio ya uhalifu yaliyoripotiwa," kimesema kikosi cha Natjoints.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.