Pata taarifa kuu

Kenya: Maandamano ya upinzani kuaanza leo Jumatatu

Nairobi – Raia nchini Kenya, hivi leo wanajiandaa kwa maandamano yaliyoitishwa na kinara wa muungano wa upinzani wa Azimio, Raila Odinga, ambaye anaînga kupanda kwa gharama za maisha na utawala wa rais William Ruto.

Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya
Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza hapo jana, Odinga alisisitiza maandamano ya hivi leo yako pale pale licha ya katazo la polisi kwenye jiji la Nairobi.

“Polisi kazi yao ni kulinda usalama wa nchi wala sio kutoa leseni, hatutatishwa na polisi.” amesema Raila Odinga.

00:19

Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya

Kwa upande wake rais Ruto, amewaonya wale aliosema watu wanaopanga kusababisha vurugu nchini humo, na kwamba serikali yake haitawavumilia wavunjifu wa amani, akimtaka Odinga kuachana na mpango wake.

“Haya maandamano na fujo na vita ni ya kuharibu mali ya watu na sisi hatutakubali hayo.” ameeleza rais Ruto

00:23

William Ruto, rais wa Kenya

Maandamano ya hivi leo ikiwa yatafanyika, yanatarajiwa kutatiza shughuli kadhaa za uma kwenye miji mingi nchi nzima.

Odinga amekuwa akisisitiza kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwezi agosti mwaka wa 2022 yakarabatiwa na tume huru ya uchaguzi nchini humo IEBC.

Viongozi wa dini na wale wa mashirka ya kiraia wametoa kwa Odinga na Ruto kufanya mazungumzo ilikulinusuri taifa kutoka katika hatari ya kutumbukia katika machafuko wakieleza kuwa wito wao umepuuzwa.

Kando na shughuli za kibiashara na uchukuzi kutatizika, wengi wanahofiwa kuwa heunda maandamano hayo yakageuka kuwa machafuko haswa wakati maofisa wa polisi wakikabiliana na wafuasi wa Odinga katika maeneo tofauti ya taifa hilo.

Hadi tukichapisha taarifa hii, hali ya utulivu ilikuwa inashuhudiwa katikati mwa jiji kuu la Nairobi, idadi kubwa ya maofisa wa polisi wakionekana katikati mwa jiji, shughuli za biashara zikionekana kutatizwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.