Pata taarifa kuu

Antony Blinken atoa wito wa 'kutunza' amani Tigray

Akiwa ziarani nchini Ethiopia ili kurejesha uhusiano wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi na Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametoa wito siku ya Jumatano 'kutunza' mchakato wa amani unaoendelea huko Tigray, kaskazini mwa nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken. AFP - OLIVIER DOULIERY
Matangazo ya kibiashara

Kudumisha mchakato wa amani. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametoa wito Jumatano, Machi 15, mjini Addis Ababa, "kutunza" mchakato wa amani unaoendelea huko Tigray, kaskazini mwa Ethiopia, wakati wa ziara inayolenga kurejesha uhusiano uliodorora na nchi hii, mshirika wa kihistoria wa Washington.

Antony Blinken ndiye afisa mkuu wa juu zaidi wa Marekani kuzuru Ethiopia tangu mwezi Novemba 2020 na kuanza kwa vita kati ya serikali ya shirikisho ya Ethiopia na mamlaka ya waasi katika eneo la Tigray, ambayo ilihitimishwa na makubaliano ya amani yaliyotiwa saini Novemba 2 huko Pretoria, Afrika Kusini.

"Kuna mengi ya kufanya. Jambo muhimu zaidi pengine ni kutunza amani ambayo inatanda kaskazini" ya nchi hiyo, ametangaza mkuu wa diplomasia ya Marekani kabla ya mkutano na mwenzake wa Ethiopia, Demeke Mekonnen, ambaye pia ni makamu - Waziri Mkuu, ambaye walichangia kahawa, jambo muhimu cha utamaduni wa Ethiopia.

Pia amesisitiza "lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Ethiopia", wakati Ethiopia iliondolewa tangu mwezi Januari 2022, Katika 'Agoa, mpango wa Marekani unaosamehe mauzo ya nje kutoka baadhi ya nchi za Afrika kutokana na kodi, kwa sababu ya mzozo huko Tigray.

"Tuna mahusiano ya zamani na ni wakati wa kuyafufua na kusonga mbele," Demeke Mekonnen alietangaza hapo awali alipokuwa akimkaribisha Antony Blinken katika ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia.

Baada ya mazungumzo, Antony Blinken alikutana na Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia tangu 2018.

"Tulikuwa na majadiliano ya kina" na "tulikubali kuimarisha uhusiano wa zamani wa nchi mbili kati ya nchi zetu, kwa ahadi ya ushirikiano", amethibitisha Abiy Ahmed kwenye Twitter.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.