Pata taarifa kuu

Tunisia: Raia kutoka mataifa ya Afrika Magharibi wanaondoka kwa kuhofia usalama wao

NAIROBI – Watu 300 kutoka mataifa ya Afrika Magharibi, nchini Tunisia, wanaondoka katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, kwa hofu ya kushambuliwa, baada ya kauli tata ya rais Kais Saied, kuhusu wakimbizi wanaokuja kwenye nchi yake. 

Watu 300 kutoka mataifa ya Afrika Magharibi, nchini Tunisia, wanaondoka katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini
Watu 300 kutoka mataifa ya Afrika Magharibi, nchini Tunisia, wanaondoka katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini REUTERS - JIHED ABIDELLAOUI
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya mwezi uliopita rais Saied, kuwaambia maafisa wa serikali kuchukua hatua za dharura, kupambana na wahamiaji haramu, akidai kuwa, kuna mpango wa wahamiaji hao, ambao ni Waafrika weusi, kutumiwa kubadilisha hali ya nchi hiyo, kuwa ya watu weusi. 

Aidha, aliwashtumu wahamiaji hao kwa kusababisha utovu wa usalama nchini humo na kutishia maisha ya raia wa Tunisia, kauli ambayo imelaaniwa na Umoja wa Afrika. 

Kundi la Kwanza la wahamiaji kutoka Guinea, wapatao 50 walirudi nyumbani siku ya Jumatano na mwishoni mwa wiki hii wale kutoka Ivory Coast na Mali wanarudi nyumbani. 

Raia hao wa kigeni wanasema wameamua kuondoka kufuatia kauli ya kiongozi wa nchi hiyo na tangu kipindi hicho wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.