Pata taarifa kuu

Uamuzi wa mahakama kuruhusu usajili wa vyama vya kutetea mashoga wapingwa Kenya

NAIROBI – Rais wa Kenya, William Ruto na kinara za upinzani Raila Odinga, kwa pamoja wameukosoa uamuzi wa mahakama ya juu, ambao ulitaka ofisi ya kusajili asasi za kiraia kutoa usajili kwa shirika la kutetea watu wanaojihusisha na ushoga, uamuzi ambao uliamsha hisia kali miongoni mwa raia na viongozi wa dini.

 William Ruto, Rais wa Kenya
William Ruto, Rais wa Kenya REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza jijini Nairobi, rais Ruto, amesema kamwe hatokubali kuona maadili ya nchi yake yanabomolewa na kwamba vitendo hivyo havitawahi kufanyika nchini Kenya.

“Mimi nataka niwaeleze yakwamba katika taifa letu la Kenya hatuwezi kwenda hiyo njia kwamba wanawake kuoa wanawake wenzao ama wanaume kuona wanaume wanzao.”amesisitiza rais Ruto.

Tangu kutolewa kwa uamuzi huo, raia wa Kenya walitumia mitandao ya kijamii kuikashifu mahakama ya juu, wakiitaka Serikali kutoruhusu masuala ya ushoga nchini mwao.

Nchini Kenya mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria uamuzi wa mahakama ukionekana kuwakera raia nchini humo.

Mataifa mengi ya Afrika hayakubali vitendo vya wapenzi wa jinsia moja nchini mwao, Uganda, taifa la Afrika Mashariki ikiwa ya hivi punde kupinga harakati za mashirika ya LGBTQ.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.