Pata taarifa kuu

Conakry yawarejesha nyumbani raia 50 wa Guinea kutoka Tunisia

Raia 50 wa Guinea wanaotaka kurejea nyumbani baada ya hatua za Tunisia dhidi ya wahamiaji haramu wako njiani kwa ndege kuelekea Conakry, afisa mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano.

Raia wa Côte d'Ivoire wanasubiri nje ya Ubalozi wa Côte d'Ivoire mjini Tunis, Februari 24, 2023.
Raia wa Côte d'Ivoire wanasubiri nje ya Ubalozi wa Côte d'Ivoire mjini Tunis, Februari 24, 2023. AFP - FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Habari hiyo imethibitishwa na afisa mkuu katika uwanja wa ndege wa Conakry. Ni safari ya kwanza ya ndege inayowarejesha nyumbani raia wa Guinea tangu hotuba ya Rais Kais Saied wa Tunisia, ambaye alitangaza wiki moja iliyopita 'hatua za dharura' dhidi ya wahamiaji haramu kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Alisema uwepo wao nchini Tunisia ni chanzo cha "vurugu, uhalifu na vitendo visivyokubalika". Katika taarifa iliyochapishwa usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, ofisi ya rais wa Guinea ilibainisha kuwa mkuu wa diplomasia, Morissanda Kouyaté, alitumwa Tunisia kwa ndege iliyokodishwa na utawala wa kijeshi "kwenda haraka kusaidia Waguinea".

Wengi wa wahamiaji 21,000 kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara waliosajiliwa rasmi nchini Tunisia, wengi wao wako katika mazingira yasiyo ya kawaida, walipoteza kazi zao (kawaida zisizo rasmi) na makazi yao kwa usiku mmoja. Wengine walikamatwa kwa ukaguzi wa polisi na wengine walishuhudia kuwa walipigwa.

Hali hii imesababisha makumi ya wahamiaji kumiminika katika balozi zao, hasa Côte d'Ivoire na Mali, wakiomba kurejea katika nchi zao. Mataifa kadhaa Kusini mwa Jangwa la Sahara yametangaza kuwarejesha nyumbani raia hao kwa hiari yao. Lakini zoezi hili la kuwarejesha raia hawa katika nchi zao litacheleweshwa na 'faini ambazo wanapaswa kulipa watu ambao wamezidisha siku za kuishi nchini Tunisia ' ambazo mara nyingi huzidi euro 1,000, alisema mwanadiplomasia wa Côte d'Ivoire.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.