Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Kundi la Islamic State lakiri kutekeleza shambulio baya nchini Burkina Faso

Kundi la wanajihadi la Islamic State (IS) limedai siku ya Ijumaa kuhusika na shambulio la kuvizia nchini Burkina Faso na kuwaua takriban wanajeshi 51 wiki iliyopita

kikosi cha wanajeshi wa Burkina Faso kikiwa mbele ya makao makuu ya televisheni ya taifa ya Burkina Faso, mjini Ouagadougou, tarehe 1 Oktoba 2022.
kikosi cha wanajeshi wa Burkina Faso kikiwa mbele ya makao makuu ya televisheni ya taifa ya Burkina Faso, mjini Ouagadougou, tarehe 1 Oktoba 2022. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa na chombo chake cha propaganda Amaq, kundi hilo limesema wapiganaji wake "walisababisha hasara kubwa kwa vikosi vya Burkina Faso katika shambulio la kuvizia lililotokea siku ya Ijumaa wiki iliyopita".

Shambulio hili la kuvizia katika eneo la Sahel linalopakana na Mali na Niger, ambalo ripoti ya awali ya vifo 51 ilitangazwa na jeshi siku ya Jumatatu, linaweza kuwa baya zaidi kuwahi kufanywa dhidi ya vikosi vya usalama tangu mwezi Novemba 2021 huko Inata (kaskazini): askari 57 waliuawa baada ya kuomba msaada bila mafanikio.

Wanajihadi hao wamesema "wameona msafara wa vikosi vya Burkina Faso ukijaribu kusonga mbele kuelekea maeneo wanayodhibiti katika mkoa wa Oudalan karibu na mpaka usio na tija na Mali". Wapiganaji wa IS "walichoma gari la kivita na kukamata gari na pikipiki 27, pamoja na makumi ya bunduki na idadi ya kubwa ya maguruneti ya kurushwa kwa roketi".

Siku ya Jumatano, watu kadhaa wa kujitolea kwa ajili ya ulinzi wa nchi hiyo (VDP), wasaidizi wa jeshi la Burkina Faso, waliuawa katika shambulio jipya la watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi kaskazini mwa nchi hiyo. Mashambulio hayo mabaya yanayohusishwa makundi ya wanajihadi yameua zaidi ya raia na wanajeshi 200 nchini Burkina Faso tangu mwanzoni mwa mwezi Januari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.