Pata taarifa kuu

Kenya: Odinga aiitisha maandamano nchi nzima kulalamikia gharama ya maisha

NAIROBI – Kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, hapo jana alitangaza kuitisha maandamano ya nchi nzima ndani ya siku 14 zijazo, ikiwa matakwa ya muungano wao wa Azimio hayatatekelezwa ikiwemo kushusha gharama ya maisha kwa raia.

Waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga
Waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga © Raila Odinga twitter
Matangazo ya kibiashara
00:25

Kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga

"Maandamano ni halali kwa hivyo tunasema kwamba watu wetu wakifanya maandamano inapaswa wapewe usalama kuhakisha kuwa wanalindwa hiyo ndio serikali ambayo imestaarabika, sisi kama wana Azimio tumesema tunataka amani katika taifa la kenya, hatutaki mtu yeyote popote atishe Mkenya.”amesema Odinga.

Hata hivyo licha ya tishio la upinzani, rais William Ruto, amepuuzilia mbali madai ya Azimio akisema nchi yao inaongozwa na utawala wa sheria na hakuna atakayemtisha mwingine.

 

00:21

Rais wa Kenya, William Ruto

“Si wanajifanya ati hao ndio majogo wa Nairobi, Nairobi gani? Nataka niwaambie watupatie nafasi ati wanataka kututisha na maandamano,watafanya maandamano mpaka watachoka.”amesisitiza William Ruto.

 

Tangu kuingia madarakani kwa serikali mpya ya rais Ruto, Odinga na wandani Wake wametangaza kutoitambua kwa kile anasema hawakushindwa kihalali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.