Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Umoja wa Afrika watangaza mkutano wa kitaifa wa maridhiano kuhusu Libya

Umoja wa Afrika (AU) umetangaza kuwa unafanyia kazi maandalizi ya mkutano ujao wa maridhiano ya kitaifa kuhusu Libya siku ya Jumapili baada ya mkutano wake wa 36 ambapo ulishikilia uamuzi wa kusimamishwa kwa nchi nne zinazoongozwa na wanajeshi katika taasisi za umoja huo.

Magari ya kijeshi kutoka kwa jeshi la Libya, watiifu kwa Abdelhamid Ddeibah, yanajiandaa kuingia katika eneo la mapigano huko Tripoli ambako mapigano kati ya wanamgambo yalitokea, Agosti 27, 2022.
Magari ya kijeshi kutoka kwa jeshi la Libya, watiifu kwa Abdelhamid Ddeibah, yanajiandaa kuingia katika eneo la mapigano huko Tripoli ambako mapigano kati ya wanamgambo yalitokea, Agosti 27, 2022. © AYMAN AL-SAHILI/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

 

"Tumekusanya pande tofauti na tunafanya kazi nao katika tarehe na mahali pa mkutano wa kitaifa" kuhusu Libya ambao utafanyika "chini ya uangalizi wa kamati ya ngazi ya juu ya Umoja wa Afrika", inayoongozwa na rais wa Congo, Denis Sassou Nguesso, Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa Tume ya AU, ameliambia shirika la habari la AFP.

Libya imetumbukia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011. Nchi hiyo inakabiliwa na mgawanyiko kati ya Mashariki na Magharibi na kuingiliwa na mataifa ya kigeni. Serikali mbili zinazohasimiana sasa zinagombea madaraka, moja ikiwa na makao yake mjini Tripoli - na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa -, nyingine huko Sirte (katikati). Mashariki na sehemu ya kusini inayodhibitiwa na Marshal Khalifa Haftar.

Uchaguzi Mkuu unaojumuisha, uchaguzi wa urais na uchaguzi wa wabunge, ulipangwa kufanyika mwezi Desemba 2021 ili kuleta utulivu nchini, umeahirishwa kwa muda usiojulikana, kutokana na tofauti kuhusu misingi ya kisheria ya uchaguzi huo na kuwepo kwa wagombea wenye utata.

"Mkutano wa maandalizi ulifanyika wiki chache zilizopita huko Tripoli", mji mkuu wa Libya, amethibitisha Bw. Faki, kabla ya kumalizia: "Mamluki wameombwa kuondoka, (...) ni muhimu kwamba Walibya waketi kwenye meza ya mazungmzo, naamini hili ni sharti la kwenda kwenye uchaguzi katika nchi yenye amani."

Kulinda Demokrasia

AU, ambayo ilihitimisha mkutano wake wa kilele wa kila mwaka siku ya Jumapili huko Addis Ababa, makao makuu ya umoja huo, ilisisitiza "kutovumilia" dhidi ya "mabadiliko yasiyo ya kikatiba" ya serikali na kushikilia amuzi wa kusimamishwa kwa Burkina Faso, Mali, Guinea na Sudan kwenye taasisi za Umoja wa Afrika. Mali, Guinea na Sudan zilisimamishwa na Umoja wa Afrika mwaka 2021, Burkina mwaka mmoja baadaye, baada ya jeshi kunyakua mamlaka.

Demokrasia lazima "ilindwe" na "kuota mizizi" na Umoja wa Afrika "unaendelea kupinga dhidi ya kuingia madarakani kwa njia isiyo ya kidemokrasia", amebainisha Bankole Adeoye, Kamishna wa AU wa Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama. Mkutano huo pia uliadhimishwa siku ya Jumamosi kwa kufukuzwa kwa mwanadiplomasia wa Israel, taifa la Kiyahudi likiituhumu Iran kuwa nyuma ya hatua hii "nzito" kwa ushirikiano a Algeria na Afrika Kusini.

Kufikia 2022, AU ilikuwa imeshindwa kufunga mijadala yake kuhusu kuidhinishwa kwa Israeli kama nchi mwaangalizi. Algeria na Afrika Kusini hasa zilibishana. Moussa Faki Mahamat alisema Jumapili kwamba idhini "ilisitishwa" kwa wakati huo na kwamba AU "haijawaalika maafisa wa Israeli" kwenye mkutano huo.

Mfumo wa kifedha 'Usio wa haki'

Viongozi wa Afrika pia walitangaza lengo la kuharakisha uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (Zlec), ambalo linapaswa kuwaleta pamoja watu bilioni 1.3. Nchi zote za AU zimesaini hilo, isipokuwa Eritrea, lakini mijadala inakwama kuhusu ratiba ya kupunguzwa kwa ushuru wa forodha, hasa kwa nchi zilizoendelea kidogo.

Kazi iliyo mbele ni "kabambe lakini inaweza kufikiwa," alisema Azali Assoumani, rais wa Comoro, kisiwa kidogo katika Bahari ya Hindi chenye wakaazi wapatao 850,000, ambaye alichukua urais wa zamu wa AU kutoka kwa Macky Sall, Rais wa Senegal. Moussa Faki Mahamat alithibitisha kuwa makubaliano haya ni ya "kimkakati", huku akielezea changamoto, katika bara ambalo watu milioni 600 hawana umeme.

Jumamosi, kabla ya mkutano mkuu wa mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alishutumu mfumo wa fedha wa kimataifa "usiofanya kazi na usio wa haki" ambao unaziona nchi za Kiafrika zikikopa fedha kwa viwango vya "kupindukia" vya riba. Kwa upande wa Bw. Guterres, anasema Afrika inakabiliwa na "changamoto kubwa (...) kwa karibu nyanja zote", inakabiliwa na athari ya migogoro ambayo haiwajibiki kwa vyovyote vile.

Antonio Guterres pia alitangaza kuwa Mfuko Mkuu wa Kukabiliana na Dharura (CERF) utatoa dola milioni 250 kusaidia watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.