Pata taarifa kuu

Sudan: Jeshi lajutia mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2021

NAIROBI – Naibu kiongozi wa Baraza la Kijeshi linaloongoza nchi ya Sudan Mohamed Hamdan Daglo amesema mapinduzi yaliyotokea mwaka 2021 yalikuwa ni kosa.

Naibu kiongozi wa Baraza la Kijeshi linaloongoza nchi ya Sudan Mohamed Hamdan Daglo
Naibu kiongozi wa Baraza la Kijeshi linaloongoza nchi ya Sudan Mohamed Hamdan Daglo ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Daglo kupitia hotuba aliyoitoa kupitia Televisheni, amesema anajuta kuwa mapinduzi hayo yamekuwa lango la kutaka kurejea madarakani kwa uongozi wa kiongozi wa zamani Omar al-Bashir.

Aidha, amesema aliungana na vuguvugu lililofanikiwa kumwondoa Bashir madarakani, lakini akakiri kufanya makosa, ya kuchukua tena madarakani Oktoba 25 mwaka 2021.

Tangu jeshi lilipoondoa uongozi wa kiraia, Sudan imeendelea kushuhudia changamoto za kisiasa na uchumi chini ya uongozi wa Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Mkuu huyo wa kikosi maalum cha jeshi kinachoogopwa, amesisitiiza utekelezwaji wa mkataba kati ya jeshi na viongozi wa mashirika ya raia uliotiwa saini Desemba tarehe tano mwaka uliopita, ili kurejesha nchi hiyo kwenye uongozi wa kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.