Pata taarifa kuu

DRC: Raia waonywa kuepuka vitendo vya kibaguzi

NAIROBI – Nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, wakati huu zoezi la kuwaandikisha wapiga kura likiendelea Mashariki mwa nchi hiyo, Gavana wa Jimbo la Kivu Kaskazini, Luteni Kanali Constant Ndima anatoa wito kwa raia katika eneo kuacha vitendo vya ubaguzi na badala yake kuvumilia kipindi hiki, baada ya madai na hofu kuwa watu wasio raia wanajiandikisha.

Zoezi la kuwaandikisha wapiga kura linaendelea nchini DRC
Zoezi la kuwaandikisha wapiga kura linaendelea nchini DRC © Laetitia Bezain - RFI
Matangazo ya kibiashara

Luteni Kanali Njike Kaiko ni msemaji wake.

“Kwa kuzingatia mvutano ambayo jimbo la Kivu Kaskazini linapitia kuhusu vita vya M23 na ADF, gavana Constant Ndima ametoa wito kwa raia wote kujiepusha na vitendo vya kudhalilisha jamii yoyote ile.” amesisitiza Luteni Kanali Njike Kaiko.  

Tume ya Uchaguzi ilianza zoezi la kuwasajili wapiga kura katika majimbo ya Mashariki mwa nchi hiyo wiki iliyopita, kuelekea uchaguzi wa mwezi Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.