Pata taarifa kuu
DRC- SIASA- UCHAGUZI

Usajili wa wapiga kura waanza mashariki mwa DRC

NAIROBI – Nchini DR Congo, kuelekea uchaguzi wa mwezi Desemba, Tume ya Uchaguzi CENI, leo inaanza zoezi la kuwaandikisha wapiga kura katika majimbo ya Mashariki mwa nchi hiyo, yanayokabiliwa na changamoto za kiusalama.

Wapiga kura wameanza kusajiliwa mashariki mwa DRC katika maeneo yanyoshudia utovu wa usalama
Wapiga kura wameanza kusajiliwa mashariki mwa DRC katika maeneo yanyoshudia utovu wa usalama © John Wessels - AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakili Paluku Kavota Pepin mwenyekiti wa mashirika ya kiraia mjini Beni, ametoa wito huu kwa wakaazi wa eneo hilo.

“Tunawaalika raia wote wa mji wa Beni kwenda kujiandikisha kama wapiga kura. ”amesisitiza Wakili Paluku Kavota Pepin mwenyekiti wa mashirika ya kiraia mjini Beni.

Baadhi ya raia katika maeneo hayo yanayokabiliwa na utovu wa usalama wamekuwa wakitaka usalama kuimarishwa ilikuwawezesha kushiriki zoezi hilo la usajili wa wapiga kura.

Raia nchini humo wanatarajiwa kushirki uchaguzi mkuu wa urais mwezi Desemba mwaka huu kuwachagua viongozi wao wapya wakiwa na matumaini kuwa uongozi mpya utasaidia katika upatikanaji wa amani êneo la mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.