Pata taarifa kuu

Eneo la Biashara Huria la Afrika kwenye ajenda ya kikao cha AU

Viongozi wa Afrika wanakutana siku ya Jumamosi na Jumapili kwa ajili ya mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Afrika (AU) kwa lengo la kuharakisha uanzishwaji wa eneo la biashara huria, katika muktadha unaobainishwa na athari za vita vya Ukraine na kuendelea kwa uasi wa kutumia silaha.

Azali Assoumani, Rais wa Comoro anatarajia kukabidhiwa kijiti cha rais wa AU, baada ya muhula wa Macky Sall kukamilika.
Azali Assoumani, Rais wa Comoro anatarajia kukabidhiwa kijiti cha rais wa AU, baada ya muhula wa Macky Sall kukamilika. AP - Frank Franklin II
Matangazo ya kibiashara

Kwa miaka mingi, viongozi wa bara hilo wamekuwa wakijadili utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (Zlecaf), ambalo litawaleta pamoja watu bilioni 1.3 na hivyo kuwa soko kubwa zaidi duniani likiwa na Pato la Taifa la Dola trilioni 3.4, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Mkutano huu wa 36 wa kilele wa AU, ambao utafanyika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, utazingatia "kuharakisha" Zlecaf. Hapo awali, soko lilipaswa kuanza kutumika kuanzia Julai 1, 2020. Lakini kufungwa kwa mipaka mingi kwa sababu ya janga la Uviko kumerudisha nyuma ratiba.

tofauti

Kwa sasa, biashara ya ndani ya Afrika inawakilisha 15% tu ya jumla ya biashara ya bara hilo. "Kuna nia ya kisiasa iliyoonyeshwa na kuthibitishwa (kuhusu eneo la biashara huria) lakini itachukua muda mrefu kuwekwa," Paul-Simon Handy, mkurugenzi wa ofisi ya Taasisi ya Mafunzo ya Usalama "Institute for Security Studies" la Addis Ababa, ameliambia shirika la habari la AFP. 

Zlec itakukuza biashara ndani ya bara na kuvutia wawekezaji, kulingana na maafisa wake. Kulingana na Benki ya Dunia, ifikapo mwaka 2035, makubaliano hayo yangeunda nafasi zaidi za kazi milioni 18 na "ingeweza kusaidia kuwainua hadi watu milioni 50 kutoka katika umaskini uliokithiri". Lakini tofauti zinabaki katika bara la Afrika.

"Zipo nchi ambazo zinasitasita kidogo katika baadhi ya mambo, hasa kuhusu itifaki ya usafirishaji huru wa watu na bidhaa. Baadhi ya nchi za Afrika zinahofia kwamba kufunguliwa kwa mipaka kutasababisha mmiminiko wa watu ambao hawawezi kuwadhibiti", anabainisha Dorine Nininahazwe, mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la ONE kutoka Afrika Mashariki, pia akitaja maswali ya ulinzi.

Nchi zote za AU, isipokuwa Eritrea, zimejiunga, lakini majadiliano yanakwama juu ya ratiba ya upunguzaji wa ushuru, hasa kwa nchi zenye maendeleo duni.

Takriban marais 35 na mawaziri wakuu wanne watahudhuria mkutano huo, kwa mujibu wa serikali ya Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.