Pata taarifa kuu
NIGERIA - USALAMA-UCHAGUZI

AU kuwatuma waangalizi wa uchaguzi nchini Nigeria

NAIROBI – Umoja wa Afrika, umetangaza kuwa utatuma ujumbe wa waangalizi wake wa uchaguzi zaidi ya 90 nchini Nigeria, wakati huu tume ya uchaguzi nchini humo, ikisema zaidi ya vituo 230 havitatumika kupigia kura kutokana na hali tete ya usalama.

Mahmood Yakubu, ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria.
Mahmood Yakubu, ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria. © The Guardian Nigeria
Matangazo ya kibiashara

Aidha tume ya uchaguzi nchini Nigeria, imeeleza kuguswa na vurugu za wakati wa mikutano ya kampeni, ikiwataka wanasiasa kujiepusha na maneno ya uchochezi.

Mahmood Yakubu, ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria.

“Tume inaguswa na vurugu wakati wa mikutano ya siasa vaina ya wafuasi wa vyama, vurugu ambazo wakati mmoja zimesababisha uharibifu wa mali na hata watu kupoteza maisha.” amesema Mahmood Yakubu

Ujumbe wa waangalizi kutoka AU utaongozwa na rais wazamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta, aliyeongoza juhudi za upatanishi nchini Ethiopia na sasa nchini DRC.

Tume hiyo imekutana na wanachama wa vyama vya kisiasa kujadili kuhusu uchaguzi ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.