Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Sitalegeza Kamba dhidi ya wanaokwepa kulipa ushuru: Rais Ruto

Rais wa Kenya, William Ruto, amesisitiza Serikali yake kutolegeza Kamba katika vita dhidi ya watu na makampuni yanayokwepa kulipa kodi, kauli ambayo hata hivyo imetafsiriwa kuwa inawalenga wapinzani wake.

Rais wa Kenya William Ruto
Rais wa Kenya William Ruto REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Kwa majuma kadhaa sasa, rais Ruto, amekuwa akirushiana maneno kuhusu kodi na wapinzani Wake, akidai suala la ulipaji kodi halitaangalia hadhi au nafasi ya mtu aliyonayo kwa jamii.

“Na mimi nimefurahi sana kwamba sasa Kenya yote tumeunganisha mawazo yetu na tumekubaliana    hakuna mkubwa wala mdogo mbele ya sheria na sisi wote tutalipa ushuru kulinagana na mapato yetu.”amesema rais Ruto.

Katika hatua nyingine, kinara wa upinzani Raila Odinga, amemkosoa Ruto kwa kile alichosema anajificha nyuma ya suala la ulipaji kodi ili kuficha utepetevu mdogo wa utendaji wa Serikali yake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.