Pata taarifa kuu
DRC- RWANDA- USALAMA

Wito wa kusitishwa kwa machafuko mashariki mwa DRC wazidi kutolewa

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, waliokutana hapo jana jijini Bujumbura Burundi, wamerudia tena wito wao wa usitishwaji mapigano kwa pande zote mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, akiteta jambo na katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dr Peter Mathuki. 04 / 02 / 2023
Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, akiteta jambo na katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dr Peter Mathuki. 04 / 02 / 2023 © Jumuiya
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo maazimio yao yamepkelewa kwa hisia tofauti na raia wa Kongo na wadadis wa mambo ambao wanaona viongozi hao wameshindwa kuwa na kauli thabiti.

Hillary Ingati, alizungumza na Francois Alwende, mchambuzi wa sias aza DRC kuhusu kikao cha jana.

Tangazo lao halikupendeza wananchi, kwa nini marais wakubali kupoteza muda wao mwingi wakati wanajua suluhisho liko wapi." amesema Francois Alwende.

Kikao hiki kimekuja wakati ambapo nchi ya DRC imekuwa ikiituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, madai ambayo Rwanda imeendelea kukanusha.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.