Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya: Upinzani watakiwa kusitisha mikutano yake ya kisiasa

Tume ya kitaifa ya maridhiano na utangamano nchini Kenya, NCIC, inamtaka kinara wa upinzani Raila Odinga, kusitisha mikutano yake ya kisiasa, tume hiyo ikisema inatumika kuwagawa Wakenya.

Raila Odinga, kiongozi wa upinzani nchini Kenya akiwa katika mkutano wa kisiasa jijini Nairobi
Raila Odinga, kiongozi wa upinzani nchini Kenya akiwa katika mkutano wa kisiasa jijini Nairobi AFP - TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Kamishena wa tume hiyo, Samuel Kona, amesema wahusika wa mikutano hiyo wamekuwa wakitoa kauli za chuki na uchochezi, ambapo ameongeza huenda wakamchukulia hatua.

“Chochote ambacho kinaweza kuwachochea wakenya au hata kuwarejesha katika hali ya kampeni na siasa zilizopita huu sio wakati wake. ”ameeleza Samwel Kona.

Wito huu unakuja wakati huu Odinga na mrengo wake wa upinzani wakitangaza misururu ya mikutano ya kisiasa wiki ijayo katika maeneo tofauti ya taifa hilo.

Odinga amekuwa akiituhumu tume ya uchaguzi nchini Kenya kwa kuhitilafiana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita na ambayo yalimpa rais Ruto ushindi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.