Pata taarifa kuu
SOMALIA- USALAMA

Viongozi wa IGAD waiunga mkono Mogadishu katika vita dhidi ya Al Shabab.

Viongozi wa ukanda wanakutana leo Jumatano jijini Mogadishu nchini Somalia, kujadili mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Al Shabab. 

Viongozi wakuu wa Jumuiya ya IGAD wakiwa katika picha ya pamoja mjini Mogadishu, Somalia. 01 / 02 / 2023
Viongozi wakuu wa Jumuiya ya IGAD wakiwa katika picha ya pamoja mjini Mogadishu, Somalia. 01 / 02 / 2023 © TheVillaSomalia
Matangazo ya kibiashara

Hali ya usalama, imeimarishwa jijini Mogadishu, huku viongozi wa mataifa ya Afrika yaliyo na vikosi vyake nchini Somalia, wakikutana kujadliana mbinu za pambano kulishinda kundi la Al Shabab. 

Viongozi kutoka Kenya, Ethiopia na Djibouti wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo. 

Mkutano huu unakuja wakati huu jeshi la Umoja wa Afrika ATMIS lilikishirikiana na lile la Somalia na makundi yenye silaha yanayoungwa mkono na serikali, yamefanikiwa kudhibiti baadhi ya mijini kutoka kwa Al Shabab. 

Umoja wa Afrika ambao una wanajeshi 20,000 unalenga, kumalizika kwa  operesheni zake kufikia mwishoni mwa  mwaka 2024 na kuacha jukumu la usalama kwa jeshi la serikali. 

Tangu alipochukua madaraka mwezi Mei mwaka uliopita, rais Hassan Sheikh Mohamud, alitangaza vita dhidi ya Al Shabab, kundi ambalo limeendelea kuwa hatari kwa usalama wa nchi hiyo na ukanda wa pembe ya Afrika. 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.