Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya: Idara ya upelelezi imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya wizi wa Kura

Idara ya upelelezi nchini Kenya, DCI, imeanzisha uchuguzi kubaini uhalali wa taarifa ya muungano wa upinzani nchini humo, Azimio la umoja unaoongozwa na Raila Odinga, kwamba rais William Ruto hakuibuka mshindi kwenye uchaguzi wa mwaka uliopita na kwamba palikuwa na wizi wa kura.

Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya
Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya © AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Odinga ametupilia mbali uchuguzi huo, akisisitiza ni lazima serikali ya rais William Ruto ijiuzulu.

“Sisi kama wana Azimio tunataka ukweli ujulikane.” amesema Raila Odinga

Odinga hivi leo amefanya mkutano kwa kisiasa jijini Nairobi wakati huu akiendelea kudai kuwa alishinda katika uchaguzi huo akitaka haki kutendeka.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.