Pata taarifa kuu
USALAMA-UGAIDI

Somalia: Bilal al-Sudani, kiongozi wa Islamic State, auawa katika shambulio la Marekani

Kiongozi wa kundi la Islamic State, aliyetambulika kama Bilal al-Sudani, na "takriban watu kumi" wanaohusishwa na kundi la kigaidi, waliuawa Jumatano katika shambulio la Marekani nchini Somalia, afisa mkuu wa Marekani alisema siku ya Alhamisi.

Mwezi Agosti mwaka uliyopita, kiongozi wa Al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri, aliuawa kwenye nyumbani kwake nchini Afghanistan na shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani.
Mwezi Agosti mwaka uliyopita, kiongozi wa Al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri, aliuawa kwenye nyumbani kwake nchini Afghanistan na shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Rais Joe Biden ameidhinisha operesheni hiyo wiki hii. Hakuna majeruhi waliorekodiwa miongoni mwa raia.

"Al-Sudani alikuwa na jukumu la kuhimiza uwepo wa kundi la Islamic State barani Afrika na kufadhili operesheni zake kote ulimwenguni, pamoja na Afghanistan," Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema katika taarifa yake.

Operesheni hii, iliyotayarishwa kwa "miezi kadhaa", haikusababisha majeruhi ama kwa raia au kati ya jeshi la Marekani, afisa mkuu wa Ikulu ya White House alisema wakati wa mahojiano na waandishi wa habari.

Rais Joe Biden aliidhinisha operesheni hiyo wiki hii, baada ya kushauriana na maafisa wa juu wa ulinzi na ujasusi, alisema.

"Hatimaye iliamuliwa kuwa kukamatwa (kwa mwanajihadi) lilikuwa chaguo bora zaidi la kupata taarifa nyingi iwezekanavyo kutokana na operesheni hiyo," afisa mwingine wa Marekani alisema. Lakini "jibu la majeshi ya adui lilisababisha kifo chake".

Afisa huyo mkuu, ambaye hakutaka kutambuliwa, alisema shambulizi hilo lilitanguliwa na "mazoezi makali" ya vikosi vya Marekani, katika maeneo "yaliyojengwa mahususi" ili kuiga eneo lilipofanyika, pango katika milima ya kaskazini mwa Somalia.

"Tulikuwa tayari kumkamata al-Sudani," alisema.

Joe "Biden ameweka wazi kwamba tumejitolea kutafuta na kuondoa vitisho vyote vya kigaidi dhidi ya Marekani na dhidi ya raia wa Marekani, popote walipo, hata katika maeneo ya mbali zaidi," afisa mwingine wa White House alisema.

Mmarekani pekee aliyejeruhiwa ni askari aliyejeruhiwa na mbwa wake wa huduma.

Jeshi la Marekani, ambalo lina kambi yake nchini Djibouti, limekuwa likifanya operesheni nchini Somalia kwa miaka kadhaa, kwa ushirikiano na jeshi la kawaida la Somalia na kwa niaba ya serikali.

Haya ni hasa mashambulizi ya anga dhidi ya waislamu wenye itikadi kali Al Shabab, wanaohusishwa na Al-Qaeda, yanayofanywa kutoka nje ya nchi, lakini pia hufanya operesheni za ardhini nchini, kati ya mbili hadi nne kwa mwaka.

Mwezi Agosti mwaka uliyopita, kiongozi wa Al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri, aliuawa kwenye nyumbani kwake nchini Afghanistan na shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.