Pata taarifa kuu

Côte d’Ivoire: Ombi la kuondoka kwa jeshi la Ufaransa nchini Burkina Faso laangaliwa kwa umakini

Nchini Côte d'Ivoire, ombi la kuondolewa kwa wanajeshi wa Ufaransa kutoka nchi jirani ya Burkina Faso, lililothibitishwa na mamlaka ya Burkina Faso mnamo Januari 23, 2023, linaangaliwa kwa umakini. "Tunapaswa kuwa waangalifu, kwa sababu kuna matatizo ya usalama na shinikizo kwenye mipaka yetu," chanzo rasmi cha Côte d’Ivoire kimeiambia RFI.

Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa Côte d'Ivoire.
Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa Côte d'Ivoire. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ya Burkina Faso alithibitisha Jumatatu Januari 23, 2023 kwamba mamlaka ya Burkina Faso imeomba kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa walioko nchini humo, ndani ya mwezi mmoja.

Nchini Côte d'Ivoire, tunafuatilia kwa karibu hali ya usalama katika ukanda wa Sahel. Na ombi hili kutoka kwa mamlaka ya Burkina Faso linaangaliwa na umakini. Hata kama huko Abidjan, uamuzi huu sio wa kushangaza.

Wakati huo huo, "hili halitutofautishi, kwa kuwa nchi zetu zimeunganishwa", hata hivyo anabaini afisa wa Côte d’Ivoire. "Tunapaswa kuwa waangalifu, kwa sababu kuna matatizo ya usalama na shinikizo kwenye mipaka yetu," kinaendelea chanzo hiki.

Côte d'Ivoire na Burkina zinatumia takriban kilomita 500 za mipaka. Kwa upande wa Côte d’Ivoire, vikosi vya ulinzi na usalama vimeimarishwa kaskazini, na miradi mingi ya maendeleo inayolenga vijana tangu wakati huo imeanzishwa kutoa njia mbadala za itikadi kali.

'Suala la uaminifu'

Ikiwa uamuzi wa Ouagadougou hautakuwa na athari za moja kwa moja kwa Côte d'Ivoire, ni uthabiti wa mapambano dhidi ya ugaidi katika kanda hiyo ambayo inaweza kupigwa. "Ikiwa Kapteni Ibrahim Traoré atathibitisha, katika wiki zijazo, ukaribu wake na Urusi, hii inaweza kusababisha tatizo la uaminifu na tatizo la upashanaji habari na Côte d'Ivoire",  anaonya Lassina Diarra, mtafiti katika Taasisi ya Timbuktu.

Hali ya Burkina Faso "ni wazi" itakuwa mada ya majadiliano kati ya Marais Emmanuel Macron na Alassane Ouattara Jumatano hii, Januari 25, amebaini mjumbe wa serikali ya Côte d’Ivoire, ambaye anakumbusha kwamba vikosi vya Ufaransa nchini Côte d'Ivoire vimekuwepo muda mrefu nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.