Tundu Lisu kurejea Tanzania Jumatano wiki hii
Nchini Tanzania, mikutano ya kisiasa, ilirejelewa tena mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kuanza kampeni zake katika ukanda wa Kaskazini kuanzia mjini Mwanza.
Imechapishwa:
Cheza - 00:36
Mikutano hii imeanza wakati huu, mwanasiasa wa upinzani Tundu Lissu ambaye amekuwa akiishi uhamishoni, akitarajiwa kurejea nyumbani, siku ya Jumatano, akitokea nchini Ubelgiji alikokuwa anaishi kwa miaka saba.
Musa Lutege ni mchambuzi wa siasa akiwa jijini Dar es salaam.
“Rais wa nchi yetu ameleta mageuzi makubwa ya siasa kupanua demokraisa ambayo ilikuwa imepitia kwenye kipindi cha giza.”amesema Musa Lutege.
Mikutano ya kisiasa ilianza nchini Tanzania, baada ya rais Samia Suluhu Hassan, kutangaza kuondoa marufuku iliyokuwa imewekwa kuzuia mikutano ya hadhara, iliyotangazwa na aliyekuwa rais Hayati John Magufuli.