Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya: Rais Ruto awaonya wapinzani

Rais wa Kenya, William Ruto, amesema serikali yake haitafumbia macho vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani vinavyopangwa na wapinzani wake, Ruto akitoa onyo hili wakati huu muungano wa kisiasa wa Azimio unaoongozwa na Raila Odinga, ukipanga kufanya maandamano na mkutano wa kisiasa hivi leo.

Rais wa Kenya William Ruto.
Rais wa Kenya William Ruto. REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Kwa majuma kadhaa rais Ruto na wapinzani wake wamekuwa wakirushiana maneno kuhusu matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana ambayo yalimpa ushindi.

“Msiwe na wasiwasi hii kenya tutaiunganisha iwe kitu kimoja, mimi siwezi ruhusu watu wachache watupangie njama ya kututisha.”amesisitiza rais Ruto

Upinzani nchini Kenya umekuwa ukidai kuwa matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana yalikarabatiwa ukiahidi kutoa ushahidi kuweka nguvu madai yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.