Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya: Raila Odinga, sitambui uongozi wa rais William Ruto

Nchini Kenya, kiongozi wa muungano wa kisiasa wa Azimio la Umoja, Raila Odinga ametangaza kuwa hamtambui William Ruto kama rais wa nchi hiyo na serikali yake, baada ya wiki iliyopita, muungano huo, kutoa ripoti inayosema ilitoka kwa wafichuzi kutoka ndani ya Tume ya uchaguzi, ikidai kuwa alimshinda Ruto kwa kura zaidi ya Milioni mbili wakati wa uchaguzi mkuu mwaka uliopita na kudai kuwa ushindi wake uliibiwa.

Waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga
Waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga © Raila Odinga twitter
Matangazo ya kibiashara

Odinga akiwahotubia wafuasi wake jijini Nairobi, baada ya kurejea nchini akitokea nchini Afrika Kusini, amesema pia hataki maridhiano yoyote ya kisiasa na rais Ruto.

“Nasema hapa leo mimi sitaki mambo ya kupeana mkono” amesema Raila Odinga.

Rais Ruto amejibu kauli ya Odinga.

“Hawa ni watu hakuna kitu wanataka ni kupeana mkono tu wanataka.” amesisitiza rais Ruto

00:28

Rais wa Kenya William Ruto akimjibu Odinga Januari 23 2023

Odinga ameendelea kusisitiza kuwa ndiye alishinda uchaguzi wa urais wa mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.