Pata taarifa kuu
MGOMO-HAKI

Wanasheria wa Misri waanza mgomo kushutumu kufungwa kwa wenzao sita

Chama cha Wanasheria wa Misri kimetangaza leo Alhamisi mgomo "bila kikomo" kushutumu kufungwa kwa wenzao sita kwa rabsha na makarani mapema mwezi huu.

Mji mkuu wa Misri, Cairo.
Mji mkuu wa Misri, Cairo. © Andrew Shenouda / GettyImages
Matangazo ya kibiashara

"Tunasitisha mara moja shughuli zetu zote, tutaacha kufika mbele ya mahakama na kushiriki katika upelelezi wa mashtaka ya umma kuanzia Januari 19 na kwa muda usio na kikomo," mawakili hao wametangaza kwenye tovuti ya chama chao.

Siku ya Jumatano, mahakama ya Marsa Matrouh (kaskazini-magharibi) iliwahukumu mawakili sita kifungo cha miaka miwili jela kufuatia mzozo uliowahusisha Januari 5 na makarani watatu wa mahakama ya mji wa pwani, kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Al-Ahram.

Wanasheria hao wa Misri wanabaini kuwa kulikuwa na "nia ya wazi ya kuwaweka wenzao kizuizini bila uhalali wa kweli" na kulaani "uamuzi wa haraka wa kuwafikisha mahakamani bila kuchukua muda wa kufanya uchunguzi wa kweli", kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Chama cha Wanasheria nchini Misri.

Mawakili wa watu sita waliopatikana na hatia wamekata rufaa dhidi ya uamuzi huo na mahakama inatarajia kuzingatia ombi lao siku ya Jumapili.

Mwezi Desemba, maelfu ya wanasheria wa Misri waliandamana nje ya makao makuu ya chama chao katikati mwa Cairo, tukio la kipekee katika nchi ambayo maandamano ya umma yamepigwa marufuku, kupinga mfumo mpya wa ankara za kielektroniki ulioanzishwa na Wizara ya Fedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.