Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya: Upinzani wadai ulishinda uchaguzi wa urais

Nchini Kenya, siku moja baada ya rais William Ruto kudai kuwa kulikuwa na mpango wa kumteka na kumuua, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati, ili kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa urais mwaka uliopita. 

Kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga
Kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga © Raila Odinga twitter
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa upinzani wa Azimio la Umoja sasa unadai umepata ripoti za ndani kutoka kwa mfanyakazi wa Tume ya Uchaguzi amabye amesema, matokeo yalibadilishwa kumpa Ruto ushindi, na mshindi halali alipaswa kuwa Raila Odinga. 

Jeremiah Kioni ni mmoja wa viongozi wa Azimio. 

“Kile ambacho kimebainishwa ni kwamba Raila alishinda uchaguzi huo kwa kupata zaidi ya kura milioni nane.”ametangaza Jeremiah Kioni.

Odinga ambaye anazuru Afrika Kusini, mara kwa mara amekuwa akisema yeye ndiye alishinda uchaguzi huo na kueleza, hivi karibuni ataeleza namna alivyoibiwa kura. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.